Hakimiliki ya picha: Getty Images
2023/24 English Premier League
Matchday 22
Liverpool v Chelsea
Anfield
Liverpool, England
Januari 31 2024, Jumatano.
Muda: Saa 4:15 usiku, majira ya Afrika ya Kati.
Liverpool wanatarajia kupata ushindi wa kwanza ndani ya
michezo sita ya ligi dhidi ya Chelsea watakapocheza Januari 31 ugani Anfield, Jumatano.
Michezo mitano ya mwisho baina ya timu hizi imeishia sare, huku Chelsea wakishinda 1-0 ugenini Machi 4 2021 baada ya the Reds kupata ushindi wa 2-0 katika mechi ya kwanza ugani Stamford Bridge Septemba 20 2020.
Vijana wa Jurgen Klopp wanaongoza jedwali la ligi baada ya ushindi wa 4-0 dhidi ya Bournemouth, Vitality Stadium Januari 21, huku Manchester City na Arsenal wakishika nafasi ya pili na tatu mtawalia baada ya ushindi wa mechi ya mchezo wa 21.
The Citizens walilaza Newcastle 3-2 ugani St James’ Park Januari 13 na the Gunners kuicharaza Crystal Palace 5-0 ugani Emirates siku saba baadaye na kukwea juu ya Aston Villa waliopo katika nafasi ya 4 baada ya kulazimisha sare ya 0-0 dhidi ya Everton, Goodison Park.
![Darwin Nunez of Liverpool Darwin Nunez of Liverpool](/medialibraries/Betway.co.tz/www-betway-co.tz/Darwin-Nunez.jpg)
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Chelsea walipata ushindi wa tatu mfululizo kwa mara ya kwanza msimu huu walipowashinda Fulham 1-0 Stamford Bridge Januari 13.
Ushindi wa nne katika michezo mitano kwa Chelsea uliwapeleka hadi nafasi ya 9 wakiwa na alama 31 sawia na Brighton ya 8. Wapo alama mbili juu ya the Magpies wanaoshikilia nafasi ya 10 na alama moja chini ya Manchester United waliopo katika nafasi 7.
Nyota ya Darwin Nunez ilionekana kung’aa na kujaza kikamilifu nafasi ya Mohamed Salah dhidi ya Bournemouth baada ya kufunga goli la kwanza dhidi yao kutokana na pasi ya Diogo Jota kabla ya kufunga goli lake la pili la mechi kutokana na pasi ya Joe Gomez. Raia huyo wa Uruguay anafikisha idadi ya magoli saba katika michezo 20 msimu huu. Inakisiwa ataendelea katika nafasi hiyo baada ya Salah kupata jeraha kwenye mashindano ya AFCON 2023 yanayoendelea nchini Ivory Coast.
![Cole Palmer of Chelsea Cole Palmer of Chelsea](/medialibraries/Betway.co.tz/www-betway-co.tz/Cole-Palmer-of-Chelsea.jpg)
Hakimiliki ya picha: Alamy
Cole Palmer anazidi kukomaa na kukua kimchezo mechi hadi mechi kwa faida ya Chelsea. Alipachika penalti kwa utulivu kabisa iliyowapa ushindi dhidi ya the Cottagers baada ya Raheem Sterling kuangushwa katika kisanduku akifuata pasi aliyotoa huyo huyo Palmer na kusababishiwa penalti. Mchezaji huyo tayari amefunga magoli 9 na kuchangia mengine 4 tangu kuhamia Chelsea akitokea Manchester City majira ya joto.
Klopp amewaasa wachezaji wake kucheza kwa umakini mwanzoni mwa mechi na kutafuta goli la mapema na baada ya timu yake kukosa kufunga goli kipindi cha kwanza dhidi ya Bournemouth.
“Tunakuwa hatari sana baada ya kutulia. Tuna sua sua tukianza mechi kama tulivyoanza leo. Tunatakiwa kuanza mechi na kuingia kwenye mfumo moja kwa moja kwa sababu sio swala la kimtazamo. Wachezaji hawa wanataka kuanza mchezo kwa kucheza vizuri,” raia huyo wa Ujerumani aliambia Sky Sports.
“Tulionyesha mchezo mzuri kipindi cha pili. Mpinzani wetu alikuwa ametulia katika mechi na nahisi hatukuanza mechi vizuri. Tuliwaruhusu wapinzani kucheza kwa masharti na kasi yao. Tulikosa utulivu na kufanya maamuzi yasiyo na tija. Tulicheza pasi ndefu tulipotakuwa kucheza pasi fupi na kucheza pasi fupi tulipotakiwa kucheza pasi ndefu.
“Tuliwapa matatizo makubwa wapinzani kupitia upande wetu wa kushoto. Habari njema ni kuwa kipindi cha kwanza kiliisha kwa sare ya 0-0. Tulibadili mfumo na ghafla tukapata mtiririko. Washambuliaji wetu walipata msaada waliohitaji. Tulikuwa watulivu kwenye kufanya maamuzi.”
Pochettino anazidi kushuhudia kikosi chake kikiimarika majuma ya hivi karibuni na amesifia umakini wao na nguvu ya kupambana kwenye dabi yao na Fulham.
“Ni muhimu kwa kikosi na juhudi zetu za kujenga mradi huu,” alisema raia huyo wa Argentina. “Ilikuwa muhimu kujiamini na kukubali kukashifiwa baada ya kichapo dhidi ya Middlesbrough (mechi ya EFL mkondo wa kwanza) kwa sababu Chelsea ni timu kubwa.
“Hiyo ni sehemu ya mchakato na matarajio ya timu kama Chelsea. Cha msingi tunaweza kukabili shinikizo na tunafahamu jinsi ya kufanya ili kufanikiwa.
“Wachezaji walikuwa makini sana leo na nilifurahishwa na dakika za kwanza 30 za kipindi cha pili. Tanahitaji kucheza hivi, kwa uhuru kwa sababu tulishirikiana vizuri.
“Hii ni timu ya wachezaji wachanga na tulizuia vizuri kwa kujituma dakika 15 za mwisho. Tulionyesha juhudi kubwa na kufanya kila lililowezekana kutetea alama tatu.”
Takwimu baina ya timu hizi, mechi 5 za mwisho za ligi.
Mechi – 5
Liverpool – 0
Chelsea – 0
Sare – 5
Ratiba ya mechi za Premier mchezo wa 22:
Januari 30, Jumanne
9:30pm: Nottingham Forest v Arsenal
9:45pm: Fulham v Everton
9:45pm: Luton Town v Brighton & Hove Albion
10:00pm: Crystal Palace v Sheffield United
10:15pm: Aston Villa v Newcastle United
Januari 31, Jumatano
9:30pm: Tottenham Hotspur v Brentford
9:30pm: Manchester City v Burnley
10:15pm: Liverpool v Chelsea
Februari 1, Alhamisi
9:30pm: West Ham United v Bournemouth
10:15pm: Wolverhampton Wanderers v Manchester United
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.