Hakimiliki ya picha: Getty Images
2023/24 English Premier League
Matchday 21
Arsenal v Crystal Palace
Emirates Stadium
London, England
Januari 20 2024, Jumamosi.
Muda: saa 9:30 mchana,
Arsenal watakabiliana na Crystal Palace kwenye mechi ya
ligi kuu England Januari 20 Jumamosi ugani Emirates nia yao ikiwa kujiweka katika nafasi ya kupigania taji la ligi hiyo.
The Gunners walikuwa na matokeo ya kutamausha mwishoni mwa mwaka 2023 baada ya kushinda mechi moja tu katika mechi tano zilizopita na kushuka hadi nafasi ya nne, alama tano nyuma ya viongozi Liverpool.
Walifikisha mechi tatu mfululizo bila ushindi walipopoteza 2-1 dhidi ya Fulham Desemba 31 na alama 40 sawia na Tottenham Hotspurs.
Manchester City walipata ushindi wa 3-2 dhidi ya Newcastle ugani St James’ Park Januari 13 na kukwea hadi nafasi ya pili, alama tatu juu ya Arsenal na vile vile juu ya Aston Villa waliotoa sare ya 0-0 na Everton uwanjani Goodison Park Januari 14.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
The Eagles walimaliza mwaka kwa matokeo mazuri walipopata ushindi wa 3-1 dhidi ya Brentford ugani Selhurst Decemba 30. Hii ni baada ya mechi nane mfululizo bila ushindi.
Palace chini ya Roy Hodgson inashikilia nafasi ya 14, alama tano juu ya nafasi ya kushuka daraja, na alama nane chini ya nafasi ya kumi.
Kuwa uwezekano wa Palace kwenda juu ya Fulham kwa ubora wa magoli iwapo watapata ushindi wa kwanza dhidi ya Arsenal katika michezo minne, baada ya kupoteza michezo mitatu ya awali dhidi yao.
Arteta anakiri timu yake inahitaji kujiweka katika hali nzuri kiakili baada ya kushuhudia matokeo mabaya ya kufunga mwaka japo anasema uchezaji wao sio tatizo.
“Ni changamoto kubwa lakini kama timu hii ingekuwa inapoteza mechi na vile vile kuonyesha mchezo mbovu na kuzembea basi ningekuwa na sababu ya kuwa na wasiwasi,” alisema raia huyo wa Uhispania.
“Nina wasiwasi kwa sababu sipendi kushindwa na sharti tushinde mechi nyingi zaidi. Tunahitaji kubadilisha hali yetu kiakili na kupata matokeo.”
Hodgson alisisitiza hakuwai kupoteza imani kwa wachezaji wake kipindi cha Novemba na Desemba walipokuwa na matokeo duni na kusema walijituma kadri ya uwezo wao chini ya hali waliyokuwa nayo.
“Tunachoamini ni kwamba tumekabiliana na hali tuliyokuwa nayo kadri ya uwezo wetu,” alisema. “Sisi kama benchi la ukufunzi hatupoteza imani na timu hii. Ni timu nzuri na tutafanya vizuri nayo. Ukweli ni kuwa hatupo kwenye hatari ya kushuka daraja.
“Kwa mtazamo mwingine, unaingia kwenye hatari ya kushuka daraja iwapo utapoteza mechi zaidi na hakuna nafasi kubwa kati yako na walio chini.”
“Usiposhinda mechi na kuzoa alama na kuanza kushuka chini kwenye jedwali lawama zitakuwa nyingi. Hiyo ndiyo hali halisi. Lazima tutafute njia ya kutatua hali hii.”
Takwimu baina ya timu hizi, mechi 5 za mwisho za ligi.
Mechi – 5
Arsenal – 3
Palace – 1
Sare – 1
Ratiba ya mechi za Premier mchezo wa 21:
Januari 20, Jumamosi
2:30pm : Arsenal v Crystal Palace
7:30pm: Brentford v Nottingham Forest
Januari 21, Jumapili
4:00pm: Sheffield United v West Ham United
6:30pm: Bournemouth v Liverpool
Januari 22, Jumatatu
9:45pm: Brighton & Hove Albion v Wolverhampton Wanderers
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.