Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022/23 English Premier League
Matchday 20
Manchester United v Manchester City
Old Trafford
Manchester, England
Saturday, 14 January 2023
Kick-off is at 14h30
Manchester United na Manchester City watamenyana katika
mechi ya ligi ugani Old Trafford Januari 14 Jumamosi, ikiwa ni dabi ya 189 baina ya timu hizo.
United wanaonekana kuimarika chini ya mkufunzi Erik ten Hag na wanatarajiwa kuwapa wakati mgumu mgumu City tofauti na hawamu ya kwanza walipochapwa 6-3 Etihad Stadium Oktoba 2.
Vijana wa Ten Hag wamepoteza alama saba tu tangu wakati huo, huku wakishinda mechi saba kati ya kumi zilizofuata na kuingia nafasi nne bora katika jedwali la ligi, na alama nne nyuma za majirani wao City.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
The Red Devils walipata ushindi wa 3-0 dhidi ya Bournemouth Jumanne ambao ulikuwa ni ushindi wa nne mfululizo na mchezo wao wa nane msimu huu bila kuruhusu goli. Mkufunzi Ten Hag anahisi kuwa wanazidi kuimarika kama kikosi na pia binafsi.
"Tupo katika nafasi nzuri. Tupo katika nafasi ambayo tunapenda lakini tutapambana hatua kwa hatua. Tunashiriki mashindano mengi kwa hivyo lengo letu ni kuzingatia mechi baada ya mechi bila kuwaza sana kitakachotokea kule mbele,” alisema.
"Tunatilia maanani juhudi tulizowekeza na tunaongeza jitihada. Mafanikio ya timu yanakuja kwanza kisha mafanikio binafsi kwa sababu timu inavyofanya vizuri ni ishara wachezaji binafsi wanaimarika vile vile.”
The Citizens walipata ushindi wa 1-0 dhidi ya Chelsea Alhamisi iliyopita kufuatia goli la Riyad Mahrez dakika ya 63.
Vijana wa Pep Guardiola hawajapoteza mechi ya ligi katika mechi tatu walizoshiriki baada ya kombe la dunia japokuwa walipata sare ya 1-1 dhidi ya Everton mkesha wa mwaka mpya.
Kufuatia sare ya 0-0 baina ya Arsenal na Newcastle Jumanne , nafasi kati ya Arsenal na City imepungua hadi alama tano tu.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Guardiola alisifia juhudi za mchezaji kinda Rico Lewis dhidi ya the Blues, alipoingia kipindi cha pili na kubadilisha mwelekeo wa mchezo.
"Kila mmoja alishuhudia kuwa kulikuwa na mabadiliko makubwa kwenye timu yetu mwanzoni mwa kipindi cha pili,” alisema. “Uchezaji wa Rico aliwezesha kila mchezaji kuwa na uhuru uwanjani. Alibadilisha mchezo kuanzia dakika ya kwanza ya kipindi cha pili.
"Ukiangalia kipindi cha pili Manu Akanji na hasa Rico ana uwezo na sifa za kuimarisha kikosi hiki. Kila mchezaji ana uwezo wa kucheza vizuri lakini alipoingia Rico, Rodri aliimarika na Kevin De Bruyne aliimarika. Kijana huyu ana kipaji kikubwa.
"Tangu ligi iliporejea amekuwa akicheza na ameongeza nguvu katika kikosi chetu ukizingatia anavyocheza kwa sasa.”
Takwimu baina ya timu hizi, mechi tano za mwisho za ligi.
Mechi - 5
Man United - 1
Man City - 3
Sare - 1
Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa​
Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za Facebook, Twitter, Instagram na Youtube. Pakua App ya Betway.