Sociedad kuikabili Bilbao inayoonekana kuimarika


Hakimiliki ya picha: Getty Images
 

2022/23 Spanish La Liga

Matchday 17

Real Sociedad v Athletic Bilbao

Estadio de Anoeta 
San Sebastian, Spain
Saturday, 14 January 2023
Kick-off is at 23h00 
 
Real Sociedad itakabiliana na Athletic Bilbao kwenye mechi ya La Liga ugani Estadio de Anoeta Januari 14.
 
The White and Blues kama inavyofahamika Sociedad walipata ushindi wa 2-0 ugenini dhidi ya UD Almeria katika mechi ya ligi iliyopita Januari 8.
 
Sociedad hawajapoteza mechi ya ligi katika michezo minne ya ligi iliyopita baada ya kuandikisha ushindi mara tatu mfululizo na kupata sare moja.

Imanol Alguacil
Hakimiliki ya picha: Getty Images 

 
Vile vile, The White and Blues hawajapoteza mchezo katika mechi mbili za ligi za mwisho wakiwa nyumbani huku wakiandikisha ushindi mmoja na sare moja ugani Estadio de Anoeta. 
 
"Tumekuwa na nafasi za kufunga magoli zaidi na kumaliza mchezo mapema,” alisema meneja wa Sociedad Imanol Alguacil baada ya mechi dhidi ya Almeria.
 
"Tulipata nafasi nyingi mchezo ukiwa 2-0 na wapinzani wetu walikuwa wanatafuta mbinu ya kupunguza idadi hiyo. Mechi ilibadilika kabisa baada ya muda wa mapumziko.
 
"Tulizembea na kuwaachia nafasi wapinzani ila juhudi za pamoja za wachezaji wetu zilituwezesha kutoruhusu goli.”
  
Kwingineko Bilbao walipata sare ya 0-0 ugenini dhidi ya Real Betis katika mechi yao ya mwisho ya ligi iliyochezwa Desemba 29 na watakuwa wenyeji wa CA Osasuna Januari 9.
 
Bilbao, maarufu kama The Lions hawajapoteza mechi ya ligi katika michezo miwili iliyopita huku wakiandikisha sare moja na ushindi mmoja.
 
Hata hivyo, Bilbao hawajapata ushindi wowote katika mechi tano za mwisho za ligi wakiwa ugenini baada ya kuandikisha sare mbili na kupoteza mechi tatu.
 
Mechi ya mwisho ya ligi baina ya Sociedad na Bilbao ilikuwa mnamo Februari 2 2022.
 
Bilbao walipata ushindi mnono wa 4-0 dhidi Sociedad katika mechi iliyoandaliwa ugani Estadio San Mames ambao ni uwanja mkubwa kabisa Basque ukiwa na uwezo wa kubeba mashabiki 53,331.
 

Takwimu baina ya timu hizi, mechi tano za mwisho za ligi.

Mechi - 5
Sociedad - 2
Bilbao - 1
Sare - 2

Ratiba ya mechi za La Liga mchezo wa 17.

 
Januari 13 Ijumaa

11:00pm- Celta Vigo v Villarreal CF

Januari 14 Jumamosi

4:00pm - Real Valladolid v Rayo Vallecano

6:15pm- Girona FC v Sevilla FC

8:30pm - CA Osasuna v Real Mallorca

11:00pm- Real Sociedad v Athletic Bilbao

Januari 15 Jumapili

4:00pm - Getafe CF v RCD Espanyol

6:15pm - UD Almeria v Atletico Madrid

Januari 16 Jumatatu

11:00pm - Cadiz CF v Elche CF
 

Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa​

Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.Chomoka na Odds


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.

 
 

Published: 01/11/2023