Reds kusaka ushindi wa kwanza katika mechi nne dhidi ya Chelsea.


Hakimiliki ya picha: Getty Images
 

2022/23 English Premier League

Matchday 21

Liverpool v Chelsea

Anfield

Liverpool, England

Saturday, 21 January 2023

Kick-off is at 14h30  

 

Liverpool watakuwa wenyeji wa Chelsea ugani Anfield katika mechi ya ligi mnamo Januari 21 siku ya Jumamosi.

 

Nafasi ya The Reds kumaliza nne bora katika ligi ilitiwa dosari walipopata kipigo cha 3-0 mikononi mwa Brighton Jumamosi iliyopita na sasa wapo alama tisa nyuma ya timu inayoshikilia nafasi ya nne katika jedwali la ligi wakiwa kwenye nafasi ya tisa.

 

Vile vile, vijana wa Jurgen Klopp walikuwa wamepoteza 3-1 dhidi ya Brentford kwenye mchezo wa ligi wa awali na sasa lengo lao ni kuepuka kupoteza mechi ya tatu ya ligi mfululizo kwa mara ya kwanza ndani ya kipindi cha miaka miwili.  


Thiago Alcantara of Liverpool
Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

Shinikizo linazidi kuongezeka kwa Klopp huku akikiri kuwa huu ni wakati ulio na changamoto kubwa katika maisha yake ya soka aliposhuhudia wachezaji wake wakizidiwa maarifa na Brighton.

 

"Matatizo yetu ni yale yale kama nilivyozungumza wiki iliyopita. Hatujitumi vilivyo katika nyakati tofauti, hatuwadhibiti wapinzani katika nyakati muhimu za mchezo na hatumiliki mpira kwa muda mrefu,” alisema raia huyo wa Ujerumani.

 

"Tulionyesha mchezo mbovu kabisa. Sio kwa timu hii ya Liverpool bali kwa ujumla. Ni wajibu wangu kurekebisha hilo. Ni wakati mgumu sana bila shaka.”

 

The Blues walipata ushindi wa 1-0 dhidi ya Crystal Palace Jumapili baada ya mechi tatu za ligi bila ushindi.

 

Haijawa rahisi kwa kocha Graham Potter ugani Stamford Bridge miezi michache iliyopita huku akishinda mechi mbili tu kati ya mechi tano alizoshiriki kabla ya mapumziko ya kombe la dunia.


Kai Havertz
Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

Chelsea wana alama 18 sawia na Liverpool ila wanachukua nafasi ya kumi kutokana na Liverpool kuwa na idadi kubwa ya mabao.

 

Potter alisifia uchezaji wa wachezaji wake huku akisema matokeo hayo yatawapa motisha ya kupambana katika mechi ijayo dhidi ya Liverpool.

 

"Kwa sasa tunashirikisha wachezaji wengi wachanga na ukizingatia hali yetu ya sasa, ni alama tatu muhimu tulizopata kutokana na juhudi tulizoonyesha kwenye mechi,” alisema.  

 

"Ni zawadi nzuri kwa wachezaji hawa na inatupa motisha kuelekea mechi ya wikendi.”

 

Takwimu baina ya timu hizi, mechi tano za mwisho za ligi.

Mechi - 5

Liverpool - 2

Chelsea - 1

Sare - 2

 

Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa​

Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.Chomoka na Odds


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.

Published: 01/20/2023