Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022/23 Italian Serie A
Matchday 20
SSC Napoli vs AS Roma
Stadio Diego Armando Maradona
Naples, Italy
Sunday, 29 January 2023
Kick-off is at 21h45
SSC Napoli itakuwa mwenyeji wa AS Roma kwenye
mechi ya ligi kuu Italia ugani Stadio Diego Armando Maradona Januari 29.
Napoli, maarufu kama The Little Donkeys ilipata ushindi wa 2-0 ugenini dhidi ya US Salernitana katika mechi iliyochezwa Januari 21.
Napoli hawajapoteza mechi yoyote ya ligi katika mechi tatu za mwisho huku wakiandikisha ushindi mara tatu mfululizo.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Vile vile, The Little Donkeys hawajapoteza mechi ya ligi katika mechi kumi na mbili za mwisho wakiwa nyumbani huku wakiandikisha sare mbili na kushinda mechi kumi ugani Stadio Diego Armando Maradona.
“Unahitaji ukakamavu wa akili na mbinu pia. Mechi sampli hii zinaweza kuathiriwa na vitu mbalimbali vya kisaikolojia lakini kikubwa zaidi ni kucheza vizuri,” alisema meneja wa Napoli Luciano Spalletti baada ya mechi dhidi ya Salernitana.
“Katika kipindi cha kwanza tulijazana sehemu moja ya uwanja hivyo basi tulikuwa katika hatari ya kupatikana na shambulizi la kushtukiza. Tuliongeza kasi ya mchezo na kufunga magoli mawili na kugeuza mwenendo wa mechi.
“Tulicheza mchezo kwa kasi yetu na utulivu kipindi cha pili ila tutahitaji kujituma zaidi na kuongeza kasi ya mchezo siku za usoni.”
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Kwingineko, Roma walipata ushindi wa 2-0 ugenini dhidi ya Spezia Calcio katika mechi ya ligi iliyopita Januari 22.
Kufuatia matokeo hayo, Roma hawajapoteza mechi ya ligi katika mechi sita za mwisho huku wakiandikisha sare tatu na ushindi mara tatu.
Vile vile, Roma hawajapoteza mchezo wa ligi katika michezo saba iliyopita wkiwa ugenini baada ya kuandikisha ushindi wa mechi tano na sare mbili.
Mchezo wa mwisho wa ligi baina ya Napoli na Roma ulikuwa Oktoba 23 2022.
Napoli walipata ushindi wa 1-0 dhidi ya Roma katika mechi iliyochezewa ugani Stadio Olimpico ambao ulifahamika kama Stadio dei Cipressi ulipoanzishwa mwaka 1927.
Takwimu baina ya timu hizi mechi tano za mwisho za ligi.
Mechi - 5
Napoli - 3
Roma - 0
Sare - 2
Ratiba ya mechi za Serie A mchezo wa 20.
Januari 27 Ijumaa
8:30pm - Bologna FC v Spezia Calcio
10:45pm - US Lecce v US Salernitana
Januari 28 Jumamosi
5:00pm - Empoli FC v Torino FC
8:00pm - US Cremonese v Inter Milan
10:45pm - Atalanta v Sampdoria
Januari 29 Jumapili
2:30pm - AC Milan v Sassuolo
5:00pm - Juventus FC v AC Monza
8:00pm - SS Lazio v ACF Fiorentina
10:45pm - SSC Napoli v AS Roma
Januari 30 Jumatatu
10:45pm - Udinese Calcio v Hellas Verona
Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa
Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.