Matsuyama atazamia kuandikisha historia shindano la Sony Open


Hakimiliki ya picha: Getty Images
 

2023 Sony Open in Hawaii

US PGA Tour

Waialae Country Club
Honolulu, Hawaii
12–15 January 2023

Bingwa mtetezi wa shindano la gofu la Sony Open in Hawaii Hideki Matsuyama anatarajiwa kushiriki shindano la mwaka huu 2023 kule Hawaii huku akitazamia kuwa mchezaji wa kwanza kushinda shindano hilo mara mbili mfululizo tangu Jimmy Walker mwaka 2014 na 2015.
 
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 atakuwa anashiriki shindano hili kwa mara ya kumi Honolulu na alimshinda Russell Henley kwenye mechi ya muondoano mwaka jana na kuandikisha ushindi wake wa nane wa PGA Tour.

Russel Henley
Hakimiliki ya picha: Getty Images 

 
Huku akiwa nyuma na mikwaju mitano na yakisalia matundu tisa tu, Matsuyama alionyesha umahiri wake kwenye raundi ya mwisho dhidi ya Henley aliposhinda mchuano huo kwenye tundu la kwanza la mchujo.
 
Mafanikio hayo yalimuweka kwenye nafasi moja na K.J. Choi ya kuwa mchezaji mwenye asili ya Asia kupata ushindi mara nyingi PGA Tour ikiwa ni mara ya kwanza tangu aliposhinda shindano la Zozo Championship Oktoba 2021.

K.J. Choi
Hakimiliki ya picha: Getty Images 

 
Akikumbuka mara ya kwanza aliposhuhudia raia huyo wa Japan akicheza, Choi alisema: “Alikuwa na ujuzi zaidi wa kucheza gofu ukilinganisha na wachezaji wengine. Alikuwa na mbinu za kipekee.
 
"Itamsaidia sana iwapo hatopata jeraha. Ni muhimu sana. Akisalia mzima wa afya na kuepuka majeraha ana uwezo wa kushinda mashindano mengi. Wachezaji wapo kwa ajili ya kuvunja rekodi. Ni furaha yangu Hideki ameafikia malengo niliyotimiza tayari.”
 
Matsuyama atakuwa mmoja wa washiriki 19 ambao pia walishiriki shindano la Sentry Tournament of Champions wiki iliyopita.
 

Washindi watano wa mwisho wa shindano la Sony Open in Hawaii.

 
2022 - Hideki Matsuyama (JPN)
2021 - Kevin Na (Marekani)
2020 - Cameron Smith (AUS)
2019 - Matt Kuchar (Marekani)
2018 - Patton Kizzire (Marekani)
 

Shinda na Kombe la Dunia

Dunia imekusanyika kushuhudia michuano bora zaidi ya soka. Ingia kwenye Droo yetu ya Kila Siku ya Mechi ujishindie TSh 500,000 na ufurahie Free Predictor.

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway. 


 

Published: 01/11/2023