Juventus wanuia kuzima moto wa Atalanta


Hakimiliki ya picha: Getty Images
 

2022/23 Italian Serie A

Matchday 19

Juventus FC v Atalanta BC 

Allianz Stadium

Torino, Italy 

Sunday, 22 January 2023 

Kick-off is at 21h45  

 

Juventus FC itakabana koo na Atalanta BC katika mechi ya ligi kuu nchini Italia ugani Allianz Stadium Januari 22.

 

Juventus ambao wanafahamika kama The Old Lady walipata kichapo kikali cha 5-1 ugenini dhidi ya Napoli kwenye mechi ya ligi iliyochezwa Januari 13.

 

Matokeo haya yalifikisha kikomo msururu wa mechi nane za ligi bila kupoteza mechi hata moja kwa upande wa Juventus kwani walikuwa wameshinda mechi zote nane mfululizo.


Gian Piero Gasperini
Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

Hata hivyo, the Old Lady hawajapoteza mechi hata moja ya ligi katika mechi 12 za mwisho wakiwa nyumbani huku wakishinda mechi nane na kwenda sare ya mechi nne.

 

Kwengineko, Atalanta walipata ushindi mnono wa 8-2 ugenini dhidi ya US Salernitana katika mechi yao ya mwisho ya ligi ya Januari 15.

 

Hivyo basi, Atalanta hawajapoteza mchezo wa ligi katika michezo mitatu iliyopita baada ya kuandikisha sare moja na kushinda mechi mbili.

 

Vile vile, Atalanta hawajapoteza mechi ya ligi katika mechi mbili za mwisho huku wakiandikisha sare moja na ushindi mmoja.

 

"Unaposhabikia ushindi kama huu ni vizuri pia kutilia maanani magoli tuliyoruhusu. Tulizembea na kuruhusu goli la kwanza kirahisi sana,” alisema kocha wa Atalanta Gian Piero Gasperini baada ya ushindi dhidi ya Salernitana.

 

"Baada ya goli hilo tulionyesha mchezo mzuri. Matokeo kama haya yanakukumbusha uwezo wa timu, kimbinu na pia kasi katika mechi tofauti.

 

"Timu hii imeonyesha uwezo wake nyakati tofauti. Leo hii tumecheza mchezo mzuri wenye kasi na kufunga magoli yenye hadhi. Matokeo yake tunapata motisha ya kuongeza juhudi katika shindano.”

 

Mechi ya mwisho ya ligi baina ya Juventus na Atalanta ilikuwa mnamo Februari 13 2022.

 

Mechi hiyo iliishia sare ya 1-1 ugani Gewiss Stadium, uwanja unaomilikiwa na Atalanta tangu mwaka 2017.

 

Takwimu baina ya timu hizi, mechi tano za mwisho za ligi.

Mechi - 5

Juventus - 0

Atalanta - 2

Sare - 3

 

Ratiba ya mechi za Serie A mchezo wa 19.


Januari 21 Jumamosi

5:00pm - Hellas Verona v US Lecce
8:00pm - US Salernitana v SSC Napoli
10:45pm - ACF Fiorentina v Torino FC

Januari 22 Jumapili

2:30pm - UC Sampdoria v Udinese Calcio
5:00pm - AC Monza v US Sassuolo
8:00pm - Spezia Calcio v AS Roma
10:45pm - Juventus FC v Atalanta BC

Januari 23 Jumatatu

8:30pm - Bologna FC v US Cremonese
10:45pm - Inter Milan v Empoli FC

Januari 24 Jumanne


10:45pm - SS Lazio v AC Milan
 

Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa​

Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.Chomoka na Odds


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.

Published: 01/20/2023