Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022/23 English FA Cup
Fourth round
Manchester City v Arsenal
Etihad Stadium
Manchester, England
Friday, 27 January 2023
Kick-off is at 23h00
Arsenal wanatarajia kuendeleza msururu wa matokeo mazuri watakapokabiliana na Manchester City kwenye
kombe la FA raundi ya nne ugani Etihad Stadium Ijumaa Januari 27.
The Gunners wamepoteza mechi moja tu ya ligi msimu huu huku wakiongoza shindano hilo alama tano zaidi ya City na wakiwa na mchezo mmoja mkononi baada ya ushindi wa 3-2 dhidi ya Manchester United wikendi iliyopita.
Hata hivyo, timu ya Mikel Arteta imekuwa na rekodi mbaya dhidi ya City hivi karibuni, ikiwa wamepoteza mechi tano za mwisho dhidi ya yao katika mashindano yote tangu walipopata ushindi wa 2-1 kwenye mechi ya nusu fainali ya FA mnamo Julai 18 2020.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Arsenal inayotoka maeneo ya Kaskazini mwa jiji la London na ambao wameshinda shindano hili mara 14 walishinda Oford United ya daraja la tatu England 3-0 katika raundi iliyopita.
Eddie Nketiah alipata goli la ushindi na la pili dhidi ya United na ameonyesha kuimarika sana tangu Gabriel Jesus kuwa majeraha huku kocha Arteta akimsifia mshambuliaji huyo.
"Eddie amemarika kupita maelezo. Tulikuwa na imani kwamba hali yake inaweza kuimarika kutokana na sifa zake zinazoingiliana na mfumo wa timu.
"Ilikuwa pigo kubwa kumpoteza Gabby (Jesus) na bado ni pigo kubwa leo hii lakini Eddie amefanya vizuri sana kujaza pengo hilo kwa njia ya kipekee.”
City wameshinda kombe hili mara sita, wakifanikiwa kufanya hivyo mara ya mwisho mwaka 2019. Waliondoa Chelsea kwenye shindano la mwaka huu kwa kuwashinda 4-0 katika mechi za raundi ya tatu.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Manchester City ya Pep Guardiola ilipata ushindi wa 4-2 dhidi ya Tottenham na 3-0 dhidi ya Wolves huku matokeo hayo yakija baada ya kupoteza 1-2 kwenye dabi dhidi ya United. Kocha huyo kutoka Uhispania anaamini timu yake itaendeleza msururu wa matokeo mazuri kwenye mechi zijazo hasa baada ya kushuhudia kiwango kizuri kutoka kwa wachezaji wake Jumapili.
"Tulizungumzia kwa kifupi mbinu zetu tunapokuwa na mpira. Hutukuzungumzia sana cha kufanya tunapopoteza mpira kwa sababu hatukuwa na nguvu,” alisema Guardiola.
"Siku hizi tunafanyia kazi kwa kifupi vitu ambavyo tunahisi hatufanyi vizuri. Huu ni mchezo mmoja tu. Tutasubiri kuona kitakachotokea siku za usoni. Tulionyesha mchezo mzuri kabisa leo. Tutasubiri kitakachotokea kwenye mechi zinazofuata.”
Takwimu baina ya timu hizi katika mechi tano za mwisho
Mechi - 5
Man City - 5
Arsenal - 0
Sare - 0
Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa​
Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.