Bees kusaka ushindi wa kwanza dhidi ya Reds ndani ya miaka 84.


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022/23 English Premier League

Matchday 19

Brentford v Liverpool

Gtech Community Stadium

London, England

Monday, 2 January 2023

Kick-off is at 20h30  

 

Brentford wanatarajia kupata ushindi kwa mara ya kwanza dhidi ya Liverpool tangu mwaka 1938 watakapokutana ugani Gtech Community Stadium Jumatatu Januari 2.

 

The Bees hawajapata ushindi dhidi ya Reds katika mechi tisa zilizopita katika mashindano yote na wamefanikiwa kushinda mara tatu tu kwenye michezo 17 ya mwisho.

 

Ushindi wa mechi hizo ulipatikana katika mfumo wa zamani wa ligi ya Premier huku ushindi wa mwisho ukija miaka 84 iliyopita walipopata ushindi wa 2-1 ugani Griffin Park mnamo Novemba 19 1938.

 

Vijana wa Thomas Frank walipata alama moja baada ya matokeo ya 2-2 dhidi ya Tottenham ligi iliporejea tarehe 26 Desemba.


Ivan Toney
Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

Vitaly Janelt (15') na Ivan Toney (54') waliipa Brentford uongozi wa 2-0 kabla ya Spurs kutoka nyuma na kufunga magoli mawili kupitia Harry Kane (65') na Pierre-Emile Hojbjerg (71') na kulazimisha sare.

 

Frank alifurahishwa na uchezaji wao dhidi ya Tottenham japokuwa anahisi timu yake ilistahili alama zote ukizingatia mchezo mzuri walioonyesha mwanzoni mwa mechi hiyo.

 

"Tulihitaji alama zote tatu katika dakika tisini,” alisema. “Hadi kufikia dakika 65 Harry Kane alipofunga tulikuwa tunafanya vizuri, tukithibiti mchezo na kutengeneza nafasi nyingi.

 

"Kasi ya mchezo ilishuka kidogo baada ya goli hilo. Bryan Mbeumo alipata nafasi nzuri ya kufunga lakini akagonga mtambaa panya kabla ya Tottenham kufunga goli la kusawazisha na kutuweka chini ya shinikizo.

 

"Kwa ujumla nimefurahishwa na uchezaji wetu. Tutanataka kufanya uwanja huu sehemu ngumu kwa wapinzani.”

 

Liverpool waliendelea kuonyesha mchezo mzuri baada ya kupata ushindi wa 3-1 dhidi ya Aston Villa Desemba 26 ugani Villa Part.

 

Liverpool ilianza mechi vizuri Mohamed Salah alipofunga goli la kwanza baada ya dakika tano. Virgil van Dijk aliongeza goli la pili dakika ya 37 kabla ya Ollie Watkins kufungia Villa dakika ya 59. Stefan Bajcetic alifunga bao la tatu kwa faida ya Liverpool mechi ikisalia dakika tisa kukamilika.


Virgil van Dijk of Liverpool
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 

Klopp anakiri kuna uwezekano hawapo mbioni kuwania taji la ligi ila anaamini wanayo nafasi kuingia katika nafasi ya kushiriki ligi ya klabu bingwa ulaya iwapo watazidi kupata matokeo mazuri.

 

"Sharti tuwakabili wapinzani wote watakaowekwa mbele yetu. Lazima tutie juhudi,” alisema.

 

"Hatupo katika nafasi nzuri. Bado kuna nafasi kati yetu na timu nyingine. Timu za kwanza mbili au tatu sio rahisi kufikia. Iwapo watashinda mechi zote zilizosalia basi hatuna nafasi hata kidogo.

 

"Tunahitaji kujituma. Jambo kubwa hapa ni kushinda mechi zetu na kuona tutakapoishia.”

 

Takwimu baina ya timu hizi, mechi zilizopita za ligi.

Mechi - 2

Brentford - 0

Liverpool - 1

Sare - 1

 

Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa​

Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.Chomoka na Odds


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.

Published: 01/02/2023