Valencia na Sevilla kumenyana katika mechi kali ya La liga


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021/22 Spanish La Liga

Matchday 21

Valencia CF v Sevilla FC 

Estadio de Mestalla
Valencia, Spain
Wednesday, 19 January 2022
Kick-off is at 22h30 
 
Valencia CF atakuwa mwenyeji wa Sevilla FC katika mechi ya La liga januari 19 ugani Estadio de Mestalla. 
 
Kwenye mechi ya januari 9, Valencia wakiwa ugenini walipigwa 4-1 na Real Madrid katika mchezo wao wa mwisho wa ligi. 
 
Valencia kwa sasa wamepoteza mechi mbili za mwisho za ligi mfululizo.

Carlos Soler
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Valencia walishindwa na Espanyol katika mechi yao ya mwisho nyumbani katika ligi matokeo ambayo yalivunja msururu wa mechi sita nyumbani bila kushindwa. 
 
"Tulikuwa na matumaini ya kupata matokeo mazuri Bernabeu hasa baada ya kupoteza mechi yetu ya awali nyumbani,” alisema kiungo wa valencia Hugo Guillamon baada ya kushindwa na Real Madrid. 
 
"Kufikia dakika ya 40 tuliwadhibiti vizuri tukisubiri kufanya shambulizi la kushtukiza. Weledi wao kabla ya kipindi cha kwanza kuisha ulitulemaza kidogo. 
 
"Walipata bao la mapema mwanzoni mwa kipindi cha pili na hilo liliharibu mipango yetu.” 

Erik Lamela
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Kwengineko Sevilla walipata ushindi mwembamba wakiwa nyumbani dhidi Getafe kwenye mechi ya ligi iliyochezwa januari 9.
 
Sevilla hawajapoteza mechi yoyote ya ligi katika mechi sita zilizopita huku wakiambulia sare moja na ushindi mara tano. 
 
Vile vile, Sevilla hawajashindwa katika mechi mbili zilizopita za ligi huku wakipata ushindi katika mechi zote mbili. 
 
Mchezo wa ligi wa mwisho baina ya timu hizi mbili ulikuwa Septemba 22 2021. 
 
Katika mchezo huo uliochezewa Estadio Ramón Sánchez Pizjuán, Sevilla waliibuka na ushndi wa 3-1.
 

Takwimu baina ya timu hizi mbili, michezo 5 ya La liga

 
Matches - 5
Valencia- 0
Sevilla - 4
Sare - 1


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 01/14/2022