Hakimiliki ya picha: Getty Images
Nigeria v Egypt
2021 Africa Cup of Nations
Group D, Matchday 1
Tuesday 11 January 2022
Roumde Adjia Stadium, Garoua
Kick-off at 19:00
Nigeria watapambana vikali na Misri kundi D, katika uwanja wa Roumde Adjia, Garoua kwenye
mashindano ya kombe la mataifa barani afrika mnamo Jumanne 11 2022. Mechi itaanza saa kumi na mbili majira ya afrika mashariki.
Nigeria ni bingwa mara tatu wa mashindano haya, mara ya mwisho ikiwa in 2013 na walimaliza katika nafasi ya tatu mwaka 2019. Nigeria walimfukuza kocha wa muda mrefu Gernot Rohr kuelekea mashindano hayo na kumuajiri Augustine Eguavoen kwa muda mfupi. Nigeria pia watakosa huduma za wachezaji nyota Emmanuel Dennis na Victor Osimhen.
Hata hivyo, Nigeria wanao uwezo wa kupigania taji hilo nchini Cameroon huku Eguavoen akitarajia kutumia fursa na muda wake hadi mwisho wa shindano hilo kupata mafanikio hayo. Baada ya mashindano hayo nafasi ya Eguavoen itachukuliwa na Jose Peseiro kwa kantarasi ya muda murefu.
“Kwa uhalisia, hakuna atakaye kuwa tayari kusikia vijisababu,” alisema Eguavoen. "Ni lazima tuwaeleze wachezaji tulipo na nafasi tunayotarajia kuwa baada ya ya shindano la AFCON. Shirikisho lina malengo, taifa lina malengo kama ilivyo kwa wachezaji na mashabiki.”
Misri ndilo taifa lenye mafanikio mengi katika mashindano ya AFCON wakiwa na mataji saba huku la mwisho likiwa la mwaka 2010. Walishika nafasi ya pili mwaka 2017 na kuondolewa katika roundi ya 16 mwaka 2019 walipokuwa wenyeji wa mashindano hayo.
Timu ya Misri ina matumaini kuwa mkufunzi wa sasa Carlos Queiroz atawatumia vizuri wachezaji na kuleta taji la nane kwa taifa hilo. Timu hiyo inajumuisha kwa kiwango kikubwa mchezaji bora duniani kwa sasa, Mohammed Salah. Licha ya yote, Carlos Queiroz anawazia sana kuhusu mechi za kufuzu kombe la dunia mwezi machi.
“Historia ya Misri katika mashindano ya AFCON ni nzuri lakini lengo letu ni kufuzu kombe la dunia. Sio malengo niliyoyaweka mimi; ya kufuzu kombe la dunia kuwa muhimu zaidi,” alisema Quieroz.
Katika takwimu baina ya mataifa haya mawili, Nigeria na Egypt wamekutana mara 18 katika mashindano yote tangu mwaka 1960. Nigeria wameshinda mara sita, Misri mara 5 huku mechi tano zikimalizika sare.
Mara ya mwisho timu hizi zilikutana katika mechi ya kirafiki mwezi Machi 2019 msini Asaba ambapo Nigeria ilishinda 1-0 Paul Onuachu akifunga goli la pekee.
Takwimu baina ya Nigeria na Egypt
Mechi: 18
Nigeria: 8
Egypt: 5
Sare: 5
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.