Hakimiliki ya picha: Getty Images
2021/22 Spanish La Liga
Matchday 20
Real Madrid v Valencia
Estadio Santiago Bernabeu
Madrid, Spain
Saturday, 8 January 2022
Kick-off is at 23h00
Real Madrid watapania kurudi na ushindi baada ya kupoteza mechi yao ya pili ya msimu katika ligi watakapoialika Valencia ugani Santiago Bernabeu januari 8.
Januari 2, Madrid walipoteza dhidi ya Getafe na kuvunja msururu wa mechi 11 za ligi bila kushindwa na sasa Sevilla inachukua nafasi ya pili nyuma yao na alama tano.
Vijana hao wa Carlo Ancelloti walikuwa wameshinda mechi nane mfululizo kabla ya kulazimishwa sare ya 0-0 na Cadiz Disemba 19.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Ancelotti hakufurahishwa na uchezaji wa timu yake na kukiri kwamba bado wachezaji wake walikuwa katika hali ya likizo ingawaje wanayo motisha ya kushinda taji namba 35 la ligi.
"Ni sharti tuchukulie kushindwa kwetu kama somo. Tupo kileleni mwa jedwali la ligi na tunafaa kuangalia mbele na uwezekano wa mafanikio,” alisema Muitaliano huyo.
"Tulimudu mchezo vizuri baada ya kufungwa lakini wasiwasi ukaingia na tukapoteza pasi kiholela na wakapata kutudhibiti vizuri katika sekta nyingi za mchezo.
"Goli lao lilitokana na makosa yetu hasa kwa mchezaji wetu mzuri sana katika safu ya ulinzi. Muonekano wetu ulikuwa na ishara kana kwamba bado tulikuwa katika likizo.”
Valencia walishuka hadi nafasi ya tisa baada ya kupoteza 2-1 dhidi ya Espanyol Disemba 31. Kabla ya mechi hii, Valencia walikuwa na msururu wa mechi tatu za ligi bila kushindwa.
Hii ilikuwa ni mechi ya kwanza kushindwa katika mechi nane za ligi baada ya matokeo mabovu mwanzoni mwa msimu ambapo walicheza mechi saba bila kushinda
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Ilikuwa ni mechi ya pili ya Jesus Vazquez kuanza msimu huu dhidi ya the Catalans na pia ilikuwa ni mechi ya kwanza kwake nyumbani. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 ana matumaini kuwa atapata nafasi nyingi ili kusaidia timu hiyo kufuzu kucheza ligi ya klabu bingwa barani ulaya, UEFA.
"Ninayo furaha kubwa sana kucheza mbele ya mashabiki wa nyumbani kwa mara ya kwanza,” alisema Vazquez. “Tulishindwa lakini tutaendelea kupambana kila uchao.
"Kwa kawaida mimi sio mtu wa kupatwa na wasiwasi lakini tukio la kuchezea katika uga wa Mastella ni mafanikio makubwa na natamani kupachezea tena.
"Matarajio yangu ni kuwa mwaka 2022 tutaimarisha nafasi yetu katika jedwali na kumaliza katika nafasi itakayotuwezesha kufuzu ligi ya UEFA.”
Takwimu baina ya timu hizi katika ligi
Mechi - 62
Real Madrid - 34
Valencia - 14
Sare - 14
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.