Rahm apania kushinda taji la Tournament of Champions


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022 Tournament of Champions

US PGA Tour

Kapalua Plantation Course
Maui
Hawaii
5–9 January 2022
 
Mchezaji namba moja wa golfu duniani Jon Rahm anapania kushinda taji la Tournament of Champions kwa mara ya kwanza kabisa. 
 
Raia huyo wa Uhispania alishinda shindano la golfu la U.S. Open la 2021 na pia ameshinda PGA tour mara sita. 
 
Rahm alimaliza msimu 2020/21 akiwa kileleni cha jedwali rasmi la dunia la golfu huku akiwa amemaliza kumi bora mara 15 na kuwa mchezaji wa kwanza kufanya hivyo tangu Dustin Johnson katika msimu wa 2015/16. 
 
Hii itakuwa mara ya kwanza kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kurejea uwanjani tangu shindano la Fortinet ambapo hakufanya vizuri. 

Justin Thomas
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Rahm alimaliza katika nafasi ya pili nyuma ya mshindi wa Tournament of Champions Dustin Johnson mwaka 2018. 
 
Harris English alishinda shindano hilo mwaka 2021 baada ya kumpiku Joaquin Niemann kwenye mchujo. Mwaka huu shindano hilo litakuwa na washindi watano wa zamani watakaoshiriki. 

Harris English
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Rahm amekiri kuwa alihitaji mapumziko madogo mwezi uliopita baada ya kuwa na ratiba ngumu ya 2021 ambapo alishiriki mashindano 21 ya PGA na European tour. 
 
Kwa sababu ya uchovu, Rahm hakushiriki shindano la mwisho la European tour, DP World Tour kule Dubai. 
 
"Baada ya majadiliano na usimamizi wangu, maamuzi ni kwamba sitokwenda Dubai wiki ijayo,” Rahm alitoa kauli. 
 
"Shughuli nyingi za msimu na changamoto zake zimenitelea uchovu mwingi. Ni muda wa kupumzika na kuwa na wakati mwema na familia yangu.” 
 

Washindi wa mashindano matano ya mwisho ya Tournament of Champions

 
2021 - Harris English (Marekani)
2020 - Justin Thomas (Marekani)
2019 - Xander Schauffele (Marekani)
2018 - Dustin Johnson (Marekani)
2017 - Justin Thomas (Marekani)
 
 

Bashiri Gofu na Betway

Ingia uwanjani mchomo mmoja ubashiri gofu na Betway. Betway inakuletea matukio yote ya gofu kutoka michuano mikubwa Duniani kote.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.


 

Published: 01/05/2022