Nigeria wataathari uwezo wa Sudan


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021 Africa Cup of Nations

Match 19, Group D

Nigeria v Sudan

Roumde Adjia Stadium
Garoua, Cameroon
Saturday, 15 January 2022
Kick-off is at 19h00  
 
Nigeria wanatarajia kushinda mchezo wao wa pili katika mashindano ya AFCON watakapoikabili Sudan ugani Roumde Adjia katika mechi ya kundi D januari 15.
 
Katika mechi ya kwanza, Nigeria waliishinda Misri 1-0 januari 11, bao la pekee likifungwa na Kelechi Iheanacho.
 
Miamba hao kutoka magharibi ya afrika wanaongoza kundi hilo kwa alama mbili baada ya Sudan na Guinea-Bissau kutoka sare ya 0-0 katika mechi yao ya kwanza ya AFCON.
 
Nigeria wanafukuzia taji la nne la mashindano haya baada ya kushinda mwaka 1980, 1994 na 2013 na hii ni mara ya 19 taifa hilo kushiriki mashindano hayo. Taifa hilo lilikosa kufika hatua ya muondoano ya mashindano hayo mara mbili tu.

Nigerian Fans
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
Eguavoen ataonyesha heshima kwa wapinzani wowote bila kujali nafasi yao katika kundi hilo ili kuepuka matokeo mabovu.
 
 “Tutacheza mechi zote kama fainali. Timu yoyote iliyofuzu kucheza mashindano haya inastahili heshima yake bila kujali jina la taifa,” alisema mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 56 baada ya mechi.
 
"Chochote kinaweza kutokea kwenye soka usipojiandaa vizuri. Sijui ni nani atakayeshinda lakini tutajaribu kwa mbinu zetu kucheza mechi zote kwa uwezo wet una jinsi inavyostahili.”
 
Sudan ina historia nzuri katika miaka ya kwanza baada ya kuasisiwa mashindano haya. Walimaliza katika nafasi ya tatu kwenye mashindano ya kwanza ya 1957, nafasi ya pili mwaka 1958 na 1963 kabla ya kushinda mashindano hayo mwaka 1970.
 
Hata hivyo, taifa hilo limefuzu mashindano hayo mara tano tangu liliposhinda taji hilo na wamefanikiwa kupita hatua ya makundi mara moja tu - 2012

 
Kocha wa Sudan Burhan Tia anasema ni muda wa taifa hilo kurudisha heshima yake katika mashindano hayo.
 
"Timu yetu ina wachezaji wa umri mdogo na tunaangalia Maisha ya usoni. Hari na uchu zitakuwa silaha kubwa sana katika mashindano haya,” Tia aliiambia CAFOnline.
 
"Chochote kinawezekana katika soka. Kundi linaweza kuwa gumu lakini kwa maandalizi mazuri tunaweza kufika hatua ya muondoano.
 
"Tunahitaji kutoa ujumbe kwamba tumeimarika na nafasi yetu iko viwango vya juu kisoka kwa sababu tumewewahi kushinda taji hili awali.”
 

Takwimu baina ya mataifa haya katika mechi tano za mwisho.

 
Mechi - 5
Nigeria - 4
Sudan - 1
Sare - 0

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 01/13/2022