Hakimiliki ya picha: Getty Images
Juventus v Napoli
2021-22 Serie A, Matchday 20
Thursday 6 January 2022
Allianz Stadium, Turin
Kick-off at 22:45
Napoli watakuwa wageni wa Juventus ugani Allianz Stadium katika
mechi ya ligi jioni ya Alhamisi januari 6 2022. Mechi itang’oa nanga saa nne kasorobo, majira ya afrika ya kati.
Juventus walianza msimu vibaya na kujikuta katika nafasi ya tano kwenye jedwali, alama nne hadi nafasi ya nne lakini wamemaliza nusu ya kwanza ya msimu vizuri kwa kujizolea alama 13 kati ya 15 katika mechi tano za mwisho. Mechi ya mwisho ilikuwa Disemba 21 dhidi Cagliari ambapo Moise Kean na Filippo Bernardeschi walikuwa wafungaji mechi hiyo ikiishia 2-0.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
“Imani bado ipo," alisema kocha wa Bianconeri Max Allegri. "Nafasi tuliyo katika ligi ni kwa sababu ya kupoteza alama dhidi ya timu kubwa. Hatuwezi kubadilisha hilo zaidi ya kushinda mechi nyingi kadri tuwezavyo.”
Kwengineko Napoli wamekuwa na matokeo mabovu wiki za mwisho wa mwaka 2021 na sasa wapo nafasi ya tatu katika jedwali alama saba nyuma ya viongozi Inter Milan. Napoli walishinda mechi moja kati ya tano za mwisho wa mwaka huku wakipoteza mechi yao ya mwisho ya 2021 1-0 wakiwa nyumbani dhidi ya Spezia, Disemba 21.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
“Tusiposhinda, waliopo nyumba yetu watatukaribia zaidi na pengine kutupita,” alisema Luciano Spalletti wa Napoli. “Tutapumzika kwa sasa kwa sababu tuna uchovu. Kumkosa Victor Osimhen kumekuwa na bahati mbaya kwa sababu safu ya ushambuliaji imekosa huduma zake. Imetubidi kubadilisha tunavyocheza ili kuvunja safu yao ya ulinzi.”
Takwimu zinaonyesha timu hizi zimekutana mara 53 katika michezo yote tangu mwaka 1993 huku Juventus wakishinda mara 27 dhidi ya 16 za Napoli ilhali mechi 10 zimetoka sare.
Timu hizi zilipokutana mwanzoni mwa msimu huu katika uwanja wa Stadio Diego Armando Maradona Septemba 2021, Napoli waliibuka na ushindi wa 2-1 mabao yaliyofungwa na Matteo Politano na Kalidou Koulibally.
Takwimu baina ya Juventus na Napoli
Matches: 53
Juventus: 27
Napoli: 16
Sare: 10
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.