Hakimiliki ya picha: Getty Images
2021/22 Italian Serie A
Matchday 23
AC Milan v Juventus
Stadio Giuseppe Meazza
Milano, Italy
Sunday, 23 January 2022
Kick-off is at 22h45
AC Milan na Juventus watachuana vikali katika
mechi ya ligi januari 23 ugani Stadio Giuseppe Meazza.
Milan waliitandika Venezia 3-0 katika mechi iliyopita ya ligi tarehe 9 januari na watakuwa wenyeji wa Spezia januari 17.
Ushindi huo dhidi ya Venezia unamaanisha Milan wameshinda mechi tatu za mwisho za ligi mfululizo.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Milan wameshinda mechi mbili za ligi kati ya tatu za mwisho wakiwa nyumbani huku mechi ya tatu wakipoteza dhidi ya Napoli ugani Stadio Giuseppe Meazza.
Kwengineko, Juventus waliishinda Udinese 2-0 wakiwa nyumbani katika mechi ya ligi iliyochezwa januari 15.
Juventus hawajapoteza mechi yoyote katika mechi nane za ligi zilizopita huku wakiambulia ushindi mara sita na sare mbili.
Juventus wameshinda mechi nne na kupata sare moja katika mechi tano zilizopita wakiwa ugenini.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
"Tulifanya vizuri katika kipindi cha kwanza. Tulifahamu wakati gani wa kushambulia na wakati wa kutulia,” alisema meneja wa Juventus Massimiliano Allegri baada ya ushindi dhidi ya Udinese.
"Kipindi cha pili hatukucheza vizuri sana na Udinese walisambaratisha mbinu zetu kabla ya Paolo Dybala kutukomboa. Ni mchezaji mzuri ambaye alitufungia goli muhimu na alikuwa na mchezo mzuri kwa ujumla.
"Ni matumaini yetu anaweza kuonyesha uwezo wake katika kipindi cha pili cha msimu,” aliendelea.
"Ukweli ni kwamba tunaendelea kuimarika katika utekelezaji wa mbinu kama vile jinsi ya kucheza na kumudu mipira mifu. Pamoja na hayo, nilitamani kushinda katika mchezo wangu wa mia tatu nikiwa kocha wa Juventus.”
Mechi ya mwisho ya ligi baina ya timu hizi ilikuwa katika uwanja wa Allianz Stadium Septemba 19 2021.
Milan wakiwa ugenini walilazimisha sare ya 1-1 dhidi ya Juventus ugani Allianz Stadium.
Takwimu baina ya timu hizi mbili katika mechi tano zilizopita za liga
Mechi - 5
Milan - 2
Juventus - 2
Sare - 1
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.