Hakimiliki ya picha: BackpagePix
2021 Africa Cup of Nations (AFCON)
Quarter-Final
Egypt vs Morocco
Stade Omnisport Ahmadou Ahidjo
Yaounde, Cameroon
Sunday, 30 January 2022
Kick-off is at 19h00
Misri itapambana na majirani wake kaskazini mwa Afrika, Morocco katika shindano la
AFCON 2021 kwenye mchezo wa robo fainali mnamo Januari 30.
Misri, maarufu kama the Pharaohs walifuzu kuingia robo fainali baada ya kuwashinda Ivory Coast katika matuta ya penalti mchezo ulipoisha sare ya 0-0 muda wa kawaida, Januari 26.
Misri wameandikisha ushindi wa mechi tatu katika mashindano haya na kupoteza mechi moja dhidi ya Nigeria.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Wamisri walipoteza mechi ya kwanza dhidi ya Nigeria na kushinda mechi dhidi ya Guinea-Bissau, Sudan na Ivory Coast.
Kwengineko, Morocco walifuzu robo fainali baada ya kuwashinda Malawi 2-1 katika mechi ya makundi mnamo Januari 25.
Morocco wameshinda mechi tatu na kutoa sare moja katika shindano hili.
Miamba hao wa Afrika Kaskazini walishinda mechi mbili mfululizo dhidi ya Ghana na Comoros kabla ya kupata sare dhidi ya Gabon kisha wakaishinda Malawi.
“Bidii na lengo letu liko pale pale, kushinda mechi zinazofuata. Tulitengeneza nafasi nyingi lakini tukazembea,” alisema kocha wa Morocco Vahid Halilhodzic baada ya ushindi dhidi ya Malawi.
"Ni matumaini yangu mchezo ufuatao tutakuwa na makali zaidi na wachezaji waliopo majeraha watakuwa wamepona na kujiunga na kikosi. Kuna majukumu makubwa yanayotusubiri.
"Tunaelewa wazi kuwa hatujafikia kiwango tunachohitaji. Naamini tutazidi kuimarika kadri tunavyocheza mechi kama hizi.”
Mara ya mwisho Misri na Morocco kukutana ilikuwa Januari 18 2017.
Morocco walipata ushindi wa 3-1 dhidi ya Misri katika mechi ya kufuzu kombe la mataifa barani Afrika mwaka 2018 ugani Stade d'Angondjé, Gabon.
Takwimu baina ya timu hizi katika mechi 29 za mwisho
Mechi - 29
Misri- 3
Morocco - 14
Sare - 12
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.