Manchester City kuendeleza ubabe wao


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021/22 English Premier League

Matchday 22

Manchester City v Chelsea

Etihad Stadium
Manchester, England
Saturday, 15 January 2022
Kick-off is at 15h30 
 
Manchester city watakuwa mwenyeji wa Chelsea katika mechi ya ligi ugani Etihad kunako januari 15 huku wakipania kuendeleza ubabe wake kwenye ligi.
 
Mabingwa watetezi City wanaongoza ligi hiyo huku nafasi kati yake na mpinzani wake wa karibu, Chelsea, ikiwa ni alama 10 baada ya michezo 21.
 
Vijana wa Guardiola walishinda Arsenal 2-1 katika mechi iliyochezwa siku ya kwanza ya mwaka huu. Ushindi huu ulikuwa wa 11 mfululizo tangu waliposhindwa 2-0 na Crystal Palace Oktoba 30.
 
Timu ya City imefunga magoli 20 katika michezo 5 na wanaongoza katika chati za ufungaji kwa magoli 53 ambayo ni moja zaidi ya Liverpool ambao bado hawajacheza mchezo mmoja.

Pep Guardiola
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Guardiola alikosa mechi ya FA dhidi Swindon januari 7 baada ya kupata maambukizi ya Korona lakini kuna uwezekano atakuwepo kwenye mechi dhidi ya Chelsea.
 
"Kama unavyofahamu Pep ndiye mkufunzi na uwepo wake una manufaa makubwa kwa timu,” kocha msaidizi wa City Rodolfo Borrell alisema kwenye tovuti ya klabu hiyo.
 
"Naamini mwanzoni mwa wiki atakuwepo kama sio mwanzo basi katikati mwa wiki.
 
"Vipimo vinaweza kuonyesha kuwa bado una maambukizi baada ya siku sita. Tuna imani wiki hii atakuwa mazoezini kuwasaidia wachezaji na maandalizi.
 
"Tutatimiza wajibu wetu. Tutafanya kila kitu pamoja na hakuna kilichobadilika. Tunayo nafasi na muda wa kujiandaa dhidi ya Chelsea.”
 
Mabingwa wa ulaya Chelsea wamepata sare katika michezo mitano mitano iliyopita. Hata hivyo, sare ya 2-2 dhidi ya Liverpool januari 2 ilihakikisha kuwa kuwa kuna alama moja katikati yao.
 
Mwezi wa Disemba, Chelsea walishinda mechi tatu na kupoteza mechi moja, ambayo ilikuwa dhidi ya West Ham.

Thomas Tuchel
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Huku mechi nyingi zikifuata, meneja wa Chelsea Tuchel aliwapumzisha wachezaji kadhaa katika mechi ya FA dhidi ya Chesterfield iliyochezwa januari 8.
 
"Kuna michezo migumu inayofuata. Kuna utofauti mkubwa unapocheza dhidi ya timu za premier na za divisheni ya tano,” alisema Tuchel baada ya ushindi wa 5-1.
 
"Lilikuwa jambo la busara kuwapumzisha baadhi ya wachezaji ili kujiweka katika hali nzuri kwa mechi zijazo. Chochote kinaweka kutokea hasa kipindi hiki cha maambukizi ya corona na kubadilisha mipango hivyo basi tunapaswa kuwa tayari kwa vyovyote vile.”
 

Takwimu baina ya timu hizi katika mechi 5 za mwisho za ligi.

Mechi - 5
Man City - 3
Chelsea - 2
Sare - 0


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 
 

Published: 01/13/2022