Juventus kukutana na Udinese huku ikiendelea kuimarika


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021/22 Italian Serie A

Matchday 22

Juventus FC v Udinese Calcio 

Allianz Stadium
Torino, Italy 
Saturday, 15 January 2022
Kick-off is at 22h00 
 
Juventus FC itachuana na Udinese Calcio katika mechi ya ligi ugani Allianz Stadium Januari 15.
 
Juventus iliibuka na ushindi wa 4-3 dhidi ya AS Roma wakiwa ugenini mnamo januari 9.
 
Ushindi dhidi ya Roma una maana kuwa Juventus imepata ushindi mara tano na sare mbili kati ya mechi saba za ligi zilizopita.

Manuel Locatelli
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Vile vile, Juventus hawajapoteza mechi yoyote kati ya mechi tatu za mwisho wakiwa nyumbani baada ya kupata ushindi mara mbili na kutoa sare moja. 
 
“Ulikuwa ni ushindi wetu sote. Tumeonyesha umoja uliopo katika kikosi chetu leo,” alisema mchezaji wa Juventus Mattia De Sciglio baada ya ushindi huo dhidi ya Roma.
 
"Tunapokuwa katika shinikizo, tunao uwezo na mbinu za kubadilisha hali hiyo lakini baada ya goli la Manuel Locatelli tulionyesha mchezo mzuri zaidi na hivyo ndivyo tulivyotakiwa kucheza kutoka mwanzoni. Hatukuonyesha mchezo mzuri katika mwanzo wa vipindi vyote viwili.
 
“Ushindi huu una maana kubwa sana kadri msimu unavyoendelea ukiwemo mchezo unaofuata ambao tutakuwa tukichezea taji la kwanza la msimu.”

Beto
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Kwingineko, Udinese walichapwa mabao 6-2 na Atalanta katika mchezo wa ligi uliochezwa januari 9.
 
Kabla ya mchezo dhidi ya Atalanta, Udinese walikuwa na ushindi mmoja na sare moja kati ya mechi mbili za ligi za awali.
 
Udinese waliishinda Cagliari katika mchezo wao wa mwisho ugenini na kuvunja msururu wa mechi saba bila ushindi wowote.
Juventus walikutana na Udinese mara ya mwisho katika ligi mnamo tarehe 22 Agosti 2021.
 
Mechi hiyo iliishia sare ya 2-2- na ilichezewa ugani Dacia Arena.
 

Takwimu baina ya timu hizi, mechi tano za mwisho za ligi

 
Mechi - 5
Juventus - 3
Udinese - 1
Sare - 1

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 
 

Published: 01/13/2022