Hakimiliki ya picha: Getty Images
2021/22 English Premier League
Matchday 23
Chelsea v Tottenham Hotspur
Stamford Bridge
London, England
Sunday, 23 January 2022
Kick-off is at 19h30
Chelsea watakuwa wenyeji wa Tottenham ugani Stamford Bridge januari 23 wakitazamia kuweka matumaini ya kushinda
ligi hai.
Chelsea walipoteza mechi dhidi ya Manchester City 1-0 januari 15 na sasa nafasi kati ya timu hizi mbili ni alama 13.
Kabla ya mechi hiyo dhidi ya City, Chelsea walikuwa wamepoteza alama muhimu kufuatia sare dhidi ya Brighton na Liverpool.
Kabla ya kukutana na City walikuwa hawajashindwa katika mechi saba za ligi ingwaje walipata sare nne kati ya mechi saba.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Mabingwa hao wa Ulaya ni miongoni mwa vilabu vilivyoathirika na visa vya maambukizi ya Covid-19 mwezi uliopita lakini ombi lao la kuahirisha baadhi ya mechi lilikataliwa na usimamizi wa ligi.
Tuchel ametaka uwazi katika mchakato wa kuahirisha mechi kwani hivi maajuzi timu nyingi zimefanikiwa kufanya hivyo kutokana na majeraha na wachezaji wao kushiriki kombe la mataifa barani afrika.
"Kwa maoni yangu tunahitaji uwazi na udhabiti katika kufanya maamuzi jambo ambalo kidogo tunalikosa,” alisema mjerumani huyo.
"Mimi sihitaji kujua kila kitu lakini pengine mashabiki wetu wanahitaji kujua. Naamini katika kanuni kwa sababu nisipofanya hivyo haileti picha nzuri.
"Vyovyote itakavyoamuliwa nitakubali kwa sababu siwezi kufanya chochote kuhusu maamuzi ambayo sina usemi nayo.”
Spurs waliathiriwa sana na maambukizi ya Covid na hawajacheza mechi yoyote ya ligi tangu waliposhinda Watford 1-0 siku ya kwanza ya mwaka.
Tottenham hawajashindwa katika mechi ya ligi chini ya uangalizi wa Antonio Conte. Ameshinda mechi tano na sare mbili katika mechi nane za kwanza na hii ni rekodi ya meneja mpya katika klabu hii. Mechi inayofuata itakuwa dhidi ya Leicester.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Conte amekiri kuwa mechi zinazofuata zitakuwa ngumu na kusema, “ni wiki ngumu inayofuata lakini tutajituma tuwezavyo kupata matokeo.”
Takwimu baina ya timu hizi katika mechi tano za mwisho za ligi
Mechi - 5
Chelsea - 4
Tottenham - 0
Sare - 1
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.