Hakimiliki ya picha: Soka La Bongo
Kocha wa Simba Fadlu Davids amesema mechi mbili zijazo zinaweza kutoa picha
halisi ya ubingwa kwa timu yake msimu huu.
Fadlu amesema kama watapoteza mechi hizo basi timu yake itakuwa imejiweka kwenye hatari kubwa ya kupoteza ubingwa, kwani itakuwa imepoteza pointi nyingi na itakuwa ngumu kumfikia aliyeko kileleni.
“Mechi kubwa zilizopo mbele yetu ni hizi za sasa dhidi ya Yanga na Coastal, hizi zingine tumeshamalizana nazo, lakini napata wakati mgumu kutokana na rekodi za mzunguko wa kwanza.
“Kwa sasa akili zipo katika mbio za ubingwa kwani bado ziko wazi na mwanga unaonekana ila tukifanya makosa mechi mbili zijazo nuru itazima kabisa.
“Hizi kwetu ni mechi zinazobeba ajenda ya ubingwa na hatutacheka nazo kabisa, kwani tunahitaji alama sita za nguvu zitakazotuweka katika nafasi nzuri.” -Amesema Fadlu davids.
MPANZU HAJIKUBALI
KATIKA Hatua nyingine Mshambuliaji wa Simba, Elie Mpanzu, licha ya kuonyesha kiwango bora, amesema bado yupo kwenye asilimia 70 ya ubora wake ndani ya kikosi cha Wekundu wa Msimbazi.
Mpanzu alijiunga na Simba katika dirisha dogo la usajili na ameanza kucheza mechi za mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ambapo ameonekana kufanya vizuri.
Akizungumza kuhusu kiwango chake, Mpanzu amesema anafurahia mchango wake ndani ya timu lakini bado hajaonyesha ubora wake wote.
"Nafurahi kuona Simba inafanya vizuri na kuwa sehemu ya wachezaji wenye mchango ndani ya timu, bado sijafikia asilimia 100 ya ubora wangu, niko kwenye 70%, ninaimani nikiendelea kupata nafasi, nitafikia kiwango ninachokitaka," amesema.
Aidha, Mpanzu amesema ana imani kuwa Simba itafanya vizuri kwenye michezo iliyosalia, kwani malengo yao ni kufanikisha kampeni ya kutwaa ubingwa.
Amezungumza pia sare waliyoipata dhidi ya Azam FC, akisema ilikuwa pigo kwao, lakini sasa wanajipanga kwa mchezo unaofuata dhidi ya Coastal Union.
"Sare dhidi ya Azam FC ilituumiza, lakini tunasonga mbele. Sasa tunajipanga kuhakikisha tunapata alama tatu dhidi ya Coastal Union,"
alisema Mpanzu.
Simba itakuwa ugenini dhidi ya Coastal Union katika mchezo utakaochezwa Jumamosi, Machi Mosi, kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.