KWA 'VIBE' HILI LA MASTAA WAPYA SIMBA...KAZI IPO LIGI KUU


HUKO Simba mambo yamezidi kunoga baada ya mastaa wapya wa kigeni waliosajiliwa katika dirisha dogo wote kutua kambini, akianza Freddy Michael Koublan kabla ya mchana wa leo Ijumaa OPa Omary Jobe na Babacar Sarr nao kutua tayari kuungana na wenzao kwenye mazoezi ya timu hiyo.
 
Freddy ni mshambuliaji kutoka Ivory Coast alioyesajiliwa akitokea Zambia, wakati Pa Jobe ni Mgambia na Sarr ni Msenegal aliyewahi kutamba na timu kadhaa ikiwamo US Monastir ya Tunisia ambao wamesajiliwa dirisha dogo lililofungwa Januari 15 sambamba na wazawa , Ladack Chasambi, Edwin Balua na Saleh Masoud Karabaka ambao wameanza mapema mazoezi tangu jana jioni.
 
Kambi ya Simba ilianza na wachjezaji ambao hawakuitwa timu ta taifa kwa ajili ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2023, ambapo kwa wale wa taifa Stars kama Mzamiru Yasin, Aishi Manula, Kibu Denis, Mohamed Hussein 'Tshabalala' tayari timu hiyo imeshatolewa kama ilivyo kwa Clatous Chama aliyekuwa na Zambia kwenye fainali hizo za Ivory Coast, huku Henock Inonga akisalia akiwa na DR Congo.
 
DR Congo inajiandaa kucheza 16 Bora ya michuano hiyo ambapo Jumapili itacheza na Misri.
 
Hata hivyo, wachezaji wa timu za taifa wanatarajiwa kuungana na wenzao kambini kumuwahi kocha Abdelhak Benchikha aliyetaka wachezaji wote kuanza kambi ya maandalizi ya mechi zijazo za Ligi Kuu Bara, Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho (ASFC).
 
Nyota wengine wa kigeni waliokuwa mapumzikoni sambamba na kina Pa Jobe na Sarr, Luis Miquissone, Saido Ntibazonkiza na Aubin Kramo ambaye ameopndoelewa kwenye sajili za ndani na kimataifa wamewahi mapema kambi hiyo.
 
Simba inayoshika nafasi ya pili katika Ligi Kuu Bara ina viporo vya mechi tano kabla ya kukamilisha duru la kwanza, huku ikisaliwa na michezo miwili ya Kundi B ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa inashika nafasi ya pili nyuma ya Asec Mimosas ya Ivory Coast, sambamba na kiporo cha ASFC dhidi ya Tembo FC.
 
Simba itaifuata Asec Februari 23 jijini Abidjan, Ivoty Coast katika mechi ya Ligi ya CAF ikiwa na kumbukumbu ya kutoka sare ya 1-1 jijini Dar es Salaam kwenye mchezo wa kwanza, kabla ya kuipokea Jwaneng Galaxy ya Botswana katika mechi ya mwisho ya kundi hilo baada ya awali kushindwa kufungana jijini Francistown, Botswana.


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.

Bashiri popote

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 01/29/2024