HII HAPA MASHINE YA KAZI ILIYOIKATAA YANGA NA KUKIMBILIA PESA ZA WAARABU


Hakimiliki ya picha: Soka La Bongo 
 


Mshambuliaji wa Medeama ya Ghana, Jonathan Sowah, ambaye alikuwa akihusishwa na Yanga dirisha dogo la usajili lililopita, amejiunga Al Nasr SC Benghazi inayoshiriki Ligi Kuu ya Libya kwa mkataba wa miaka mitatu.
 
Sowah alihusishwa na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara kutokana na kiwango alichokionyesha kwenye mechi za makundi Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu ikiwa kundi moja na Yanga na presha aliyoionyesha kwenye mchezo dhidi yao, ikiwamo bao la penalti aliwashawishi mabosi wa timu hiyo kufikiria kumsajili.
 
Sowah aliisumbua pia safu ya ulinzi ya vijana wa Miguel Gamondi iliyokuwa chini na nahodha Bakar Mwamnyeto, Ibrahim Bacca na Dickson Job na kwa mujibu wa Ghanasoccernet.com, Al Nasr ilimvuta mshambuliaji huyo anayekiwasha kwa mabingwa wa Ligi Kuu ya Ghana kwa dili la nono baada ya mazungumzo yaliyozaa matunda kati ya timu hizo mbili na kufuta kabisa uwezekano wa kutua Jangwani hata mwisho wa msimu.
 
Sowah (25) akiwa na rekodi nzuri amefunga mabao 19 katika mechi 35 tangu msimu uliopita na anaendelea kudhihirisha uwezo wake wa kupachika mabao huku msimu huu akiwa amefunga mabao saba katika mechi 15 za Ligi Kuu ya Ghana, yakiwemo matatu katika ya Ligi ya Mabingwa ya Afrika.
 
Kiwango chake kizuri kimemfanya apate nafasi katika kikosi cha mwisho cha Ghana kwenye fainali za Mataifa Afrika 2023, zinaloendelea nchini Ivory Coast huku timu hiyo ikiwa imetolewa kwenye hatua ya makundi.
 
Sowah alicheza mechi yake ya kwanza ya ushindani kwa Black Stars wakati wa kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia 2026 dhidi ya Comoro na kupoteza bao 1-0.


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.

Bashiri popote

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.

Published: 02/02/2024