Alamy Foto
2023/24 English Premier League
Matchday 26
Manchester United v Fulham
Old Trafford
Manchester, England
Jumamosi, Februari 24 2024
Muda: Saa 10:00
Manchester United wanapania ushindi wa tano mfululizo kwenye
ligi kwa mara ya kwanza ndani ya miezi 13 watakapowakaribisha Fulham ugani Old Trafford Jumamosi Februari 24.
The Red Devils walipata ushindi wa 2-1 dhidi ya Luton ugani Kenilworth Road Jumapili iliyopita, Februari 18 Rasmus Hojlund alipofunga magoli mawili dakika za kwanza saba za mchezo na kupata ushindi wa nne mfululizo kwenye ligi.
Vijana wa Erik ten Hag hawajafanikiwa kushinda mechi tano mfululizo tangu walipopata ushindi wa 2-1 nyumbani dhidi ya Manchester City mnamo Januari 14 2023.
United wanashikilia nafasi ya 6 kwenye msimamo wa ligi, alama tatu nyuma ya Tottenham ambao walipoteza 2-1 kwenye mchezo wao na Wolves ugani Tottenham Hotspur Stadium Jumamosi Februari 17. Aston Villa walikwea hadi nafasi ya 4 baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Fulham ugani Craven Cottage.
Fulham wamepata alama tano tu katika michezo mitano ya ligi iliyopita lakini walikuwa hawajapoteza mchezo hata mmoja katika michezo mitatu ya awali kabla ya kukutana na Aston Villa.
Fulham chini ya Marco Silva wanashikilia nafasi ya 12 kwenye jedwali, nyuma ya Wolves na Chelsea wanaoshika nafasi ya 11 na 10 mtawalia.
Bournemouth wapo katika nafasi ya 13 baada ya sare yao ya 2-2 dhidi ya Newcastle ugani St James' Park ikiwa ni mwendelezo wa matokeo yao duni.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Katika taarifa za kikosi, idadi ya majeruhi kwenye kikosi cha United inazidi kukua baada ya mlinzi wa kushoto Luke Shaw kupata jeraha dhidi ya the Hatters wikendi iliyopita na anaungana na Lisandro Martinez, Tyrell Malacia, Aaron Wan-Bissaka, Anthony Martial na Mason Mount kwenye orodha hiyo. Raul Jimenez atakosa mechi hiyo kwa upande wa Fulham huku Kenny Tete na Armando Broja wakitarajiwa kurejea mchezoni Old Trafford baada ya kukosa mechi iliyopita.
Hojlund amefanikiwa kufunga magoli saba katika michezo saba iliyopita kwa faida ya United na kocha wake Ten Hag anaamini kuwa mchezaji huyo ataendelea na kasi hiyo ya ufungaji.
"Tulimsajili kwa kuwa na uwezo mkubwa kiakili. Licha ya kuwa na umri wa miaka 21 anaweza kufanya vizuri chini ya shinikizo. Ni sifa inayohitajika kuwa mshambuliaji wa Manchester United," raia huyo wa Uholanzi aliambia kituo cha habari cha Sky Sports.
"Anajiamini muda wote hata anapokuwa hafungi magoli. Ufungaji wake wa magoli umeimarika na msururu huo utaendelea. Ni sifa moja yake. Anajiamini sana. Ni imani yangu atazidi kufunga magoli.”
Silva alihisi hakukuwa na tofauti kubwa kati yao na Villa katika mchezo huo lakini akakiri kuwa waliruhusu magoli mawili kizembe.
"Tulifahamu jinsi gani ya kucheza na mbinu za kutumia kupata matokeo mazuri dhidi ya Villa lakini tuliruhusu magoli kirahisi sana,” alisema raia huyo wa Ureno.
"Sharti uwe makini sana unapocheza dhidi ya timu kama hizi, dhidi ya washambuliaji na wafungaji kama hawa lakini tulikosa umakini huo. Bahati mbaya malipo yake yalikuwa kupoteza mechi hiyo.
"Kwa ujumla, ukitazama uchezaji wa timu zote mbili, kujituma kwao na kujiamini kwenye mchezo hakukuwa na tofauti kubwa kwa kweli.
"Hatukuweza kufunga kutokana na nafasi tulizotengeneza na tuliruhusu magoli mawili kirahisi. Hata hivyo wachezaji wangu walipambana hadi kipenga cha mwisho. Walizidi kujiamini, kujituma na walikuwa na uchu wa kupata matokeo mazuri.”
Takwimu baina ya timu hizi, mechi tano za mwisho za ligi.
Mechi - 5
Man United - 4
Fulham - 0
Sare - 1
Ratiba ya mechi za Premier mchezo wa 26:
Februari 21 Jumatano
9:30pm: Liverpool v Luton Town
Februari 24 Jumamosi
5:00pm: Aston Villa v Nottingham Forest
5:00pm: Brighton & Hove Albion v Everton
5:00pm: Crystal Palace v Burnley
5:00pm: Manchester United v Fulham
7:30pm: Bournemouth v Manchester City
10:00pm: Arsenal v Newcastle United
Februari 25 Jumapili
3:30pm: Wolverhampton Wanderers v Sheffield United
Februari 26 Jumatatu
10:00pm: West Ham United v Brentford
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.