EPL - Manchester City v Everton


Alamy Foto


2023/24 English Premier League
Matchday 24
Manchester City v Everton
Etihad Stadium
Manchester, England
Jumamosi, Februari 10 2024
Muda: Saa 8:30 mchana majira ya Afrika ya Kati.
 
Manchester City watakuwa na nafasi ya kuchukua uongozi wa ligi japo kwa muda mchache watakapoalika Everton ugani Etihad mapema Jumamosi Februari 10.
 
The Citizens walipata ushindi wa 3-1 dhidi ya Brentford ugani Gtech Community na kupunguza alama kati yao na Liverpool hadi mbili mnamo Februari 5.
 
Msururu wa mechi 15 bila kupoteza kwa the Reds ulifika kikomo Jumapili Februari 4 waliposhindwa 3-1 na Arsenal uwanjani Emirates.
 
City wanashikilia nafasi ya 2 kwenye jedwali, mbele ya Arsenal kwa ubora wa magoli inayoshikilia nafasi ya 3 japo wamecheza mchezo mmoja zaidi ya City. 

Phil Foden
Hakimiliki ya picha: Getty Images 

 
Aston Villa walikwea hadi nafasi ya 4 baada ya kuilaza Sheffield United 5-0 uwanjani Bramall Lane mnamo Februari 3 na kuipiku Tottenham ambao walitoa sare ya 2-2 na Everton Goodson Park.
 
Sare ya tatu mfululizo kwenye mechi za ligi kwa Everton chini ya Sean Dyche imewaacha katika nafasi ya 18, alama moja chini ya nafasi za kushushwa daraja. Hii ni baada ya Luton iliyopo nafasi ya 17 kutoa sare ya 4-4 dhidi ya Newcastle United uwanjani St James' Park. Burnley wapo katika nafasi ya 19 baada ya kulazimisha sare ya 2-2 dhidi ya Fulham, Turf Moor.
 
Katika habari za kikosi, timu ya Guardiola haina majeruhi yeyote baada ya mshambuliaji Erling Haaland kumaliza mchezo wao dhidi ya the Bees bila maumivu yoyote. Ulikuwa ni mchezo wake wa kwanza tangu kupata jeraha la mguu na kukosa mechi tano. Kwingineko, Dyche anawakosa wachezaji kadhaa akiwemo Arnaut Danjuma anayeuguza jeraha la kifundo cha mguu, Dele Alli anauguza kinena na na Andre Gomes anayeuguza jeraha la mguu. Hata hivyo, kuna uwezekano wa Abdoulaye Doucoure anayeuguza jeraha la paja, Amadou Onana anayeuguza jeraha la goti na Ben Godfrey anayeuguza jeraha la mguu kushiriki mechi hiyo.
   
Guardiola alikuwa na sifa tele kwa Phili Foden ambaye alifunga magoli matatu dhidi ya Brentford, akitaja umuhimu wake kwenye kikosi cha City msimu huu.
 
"Nilisema wiki chache zizilizopita kuwa Phil ana mchango mkubwa katika kikosi msimu huu hasa ukizingatia magoli na mchango wa magoli,” alisema raia huyo wa Uhispania.
 
"Amekuwa na mchango mkubwa kwetu msimu huu. Anaelewa mchezo vizuri. Mchezo wake ni maarifa na kasi vile vile. Muda wote ana hatari ya kufunga magoli na kuwatatiza walinzi wa timu pinzani eneo la kisanduku. Yupo maeneo hayo muda wote.
 
"Anajua kujiweka katika maeneo mazuri ya kupokea pasi. Anajituma sana kwa ajili ya timu. Ni mchezaji wa kipekee. Amecheza mechi 250 au zaidi katika kikosi cha City kwa umri wake. Ni ishara kuwa amekuwa na ushawishi mkubwa tangu ameanza kucheza kwenye kikosi hiki.”
 
Dyche alisifia juhudu za wachezaje wake baada ya kutoka magoli mawili nyuma na kulazimisha sare dhidi ya Spurs. Kocha huyo anaamini kuna ishara tosha za kuimarika katika azma yao ya kuepuka kushuka daraja.
 
"Nilishuhudia mambo mengi ya kuridhisha na juhudi nyingi za timu hii. Ni kipimo muhimu cha kazi yetu ya msimu. Hata tunapokuwa chini ya shinikizo, tunazidi kuamini kwenye uwezo we,” alisema.
 
"Kuna ishara nzuri kuafikia malengo tuliyonayo hapa licha ya changamoto tunazopitia na mashaka ya wengi.”
 

Takwimu baina ya timu hizi, mechi 5 za mwisho za ligi.

Mechi - 5
Man City - 4
Everton - 0
Sare - 1
 

Ratiba ya mechi za Premier mchezo wa 24:

 
Februari 10 Jumamosi
 
2:30pm: Manchester City v Everton
 
5:00pm: Fulham v Bournemouth
 
5:00pm: Liverpool v Burnley
 
5:00pm: Luton Town v Sheffield United
 
5:00pm: Tottenham Hotspur v Brighton & Hove Albion
 
5:00pm: Wolverhampton Wanderers v Brentford
 
7:30pm: Nottingham Forest v Newcastle United
 
Februari 11 Jumapili
 
4:00pm: West Ham United v Arsenal
 
6:30pm: Aston Villa v Manchester United
 
Februari 12 Jumatatu
 
10:00pm: Crystal Palace v Chelsea


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.

Bashiri popote

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 
 

Published: 02/09/2024