EPL - Everton v Tottenham Hotspur


Alamy Foto


2023/24 English Premier League
Matchday 23
Everton v Tottenham Hotspur
Goodison Park
Liverpool, England
Jumamosi Februari 3 2024.
Muda: saa 8:30 mchana majira ya Afrika ya Kati.
 
Tottenham watamenyana na Everton kwenye mechi ya ligi kuu England ugani Goodison Park Jumamosi Februari 3.  
 
Spurs walikwea hadi nne bora kwenye jedwali la ligi baada ya ushindi wa 3-2 dhidi ya Brentford ugani Tottenham Hotspur Januari 31 na kushuhudia Aston Villa wakipoteza 3-1 dhidi ya Newcastle ugani Villa Park siku moja kabla.  
 
Spurs chini ya Ange Postecoglou wanachukua nafasi ya 5, sawia na Aston Villa wenye alama 43 lakini wana ubora wa mabao. Arsenal wanashikilia nafasi ya 3 wakiwa na alama 46, Manchester City wapo katika nafasi ya 2 huku Liverpool wakishika nafasi ya kwanza.
  
The Toffees wapo katika hatari ya kushuka daraja baada ya kutoa sare ya 0-0 na Fulham ugani Craven Cottage Januari 30, mechi iliyofikisha msururu wa mechi tano za ligi bila ushindi.
 
Luton walikwea hadi nafasi ya 17 baada ya ushindi wa kushangaza wa 4-0 dhidi ya Brighton uwanjani Kenilworth, Burnley wapo katika nafasi ya 19 huku Sheffield United wakivuta mkia baada ya kupoteza dhidi ya Manchester City na Crystal Palace mtawalia katikati mwa juma.
 
Sean Dyche alikosa huduma za viungo wengi kwenye mechi yao dhidi yao Fulham na aliwasifia wachezaji wake kwa kupata alama moja muhimu katika mazingira na changamoto hizo.
 
"Ukizingatia changamoto tulizo nazo za majeraha, nimefurahishwa na alama moja tuliyopata na pia kwa kutoruhusu goli,” Dyche aliambia evertontv. "Tulizuia kwa pamoja kama timu.
 
"Sio jambo rahisi hasa unapokosa wachezaji wazoefu ambao wameonyesha kuwa wanaweza kuwa msaada mkubwa kwenye timu na kukosa suluhu la haraka. Nimefurahishwa na juhudi za waliocheza kwani walikuwa na nia ya kushinda mechi hii.”

RicharlisonHakimiliki ya picha: Getty Images 

 
Postecoglou alifurahishwa na uchezaji wa timu yake kipindi cha pili baada ya kukosa umakini na kuruhusu goli dakika ya 15 ya mchezo, the Bees walipochukua uongozi wa mechi kupitia Neal Maupay.
 
"Vijana walionyesha juhudi na kupata alama tatu. Hata hivyo tumeimarika sana,” aliambia SPURSPLAY. "Kikosi chetu bado ni kichanga. Tunajaribu kukuza na kutafuta mbinu mwafaka zitakazofaa timu hii. Tunategemea wapinzani watatupa changamoto tofauti katika mchakato huu.
 
"Hatukucheza vizuri kipindi cha kwanza kama nilivyosema lakini tulijitahidi na kugeuza takwimu kipindi cha pili.”
 

Takwimu baina ya timu hizi, mechi tano za mwisho za ligi.

Mechi - 5
Everton - 0
Tottenham - 3
sare - 2
 

Ratiba ya mechi za Premier League mchezo wa 23:

 
Februari 3 Jumamosi
 
2:30pm: Everton v Tottenham Hotspur
 
5:00pm: Brighton & Hove Albion v Crystal Palace
 
5:00pm: Burnley v Fulham
 
5:00pm: Newcastle United v Luton Town
 
7:30pm: Sheffield United v Aston Villa
 
Februari 4 Jumapili
 
4:00pm: Bournemouth v Nottingham Forest
 
4:00pm: Chelsea v Wolverhampton Wanderers
 
4:00pm: Manchester United v West Ham United
 
6:30pm: Arsenal v Liverpool
 
Monday, February 5
 
10:00pm: Brentford v Manchester City


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.

Bashiri popote

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 02/02/2024