KOCHA Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi ameshusha presha, na kusema sasa ana matumaini makubwa ya kufanya vyema
katika mechi zinazofuata baada ya kurejea kwa wachezaji wake tegemeo, Djigui Diarra na Stephane Aziz Ki.
Gamondi amesema hata wachezaji wake sasa watatulia, hawatocheza kwa presha kama michezo kadhaa iliyopita ambapo walikuwa wakishinda kwa mbinde kutokana na kutokuwa na baadhi ya wachezaji tegemeo kwenye kikosi.
Nyota hao hawao hawakuwepo katika michezo mitatu ambayo Yanga wamecheza kulingana na kuwepo kwenye majukumu ya timu zao za Taifa katika michuano ya fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON), Diarra akiwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Mali, na Aziz Ki, Burkina Faso, lakini sasa wamerejea na kutarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha mchezo wa kesho kutwa.
Yanga kesho watakuwa na kibarua kigumu mbele ya wenyeji wao KMC FC katika uwanja wa Jamhuri, Morogoro ambapo mechi ya mzunguko wa kwanza waliibuka na ushindi wa mabao 5-0.
Kocha Gamondi amesema amefanyia kazi mapungufu yao yao lakini kurejea kwa nyota hao wawili anaimani kutarejesha ridhimu ya kikosi chake na kutocheza kwa presha kubwa.
Amesema licha ya kila mchezaji ndani ya kikosi chake kuwa muhimu lakini anaimani kurejea kwa Aziz Ki na kipa wake kutarejesha upambanaji wa timu kwa sababu kuna kitu kitakuwa kimeongezeka.
“Ni jambo la furaha kurejea kikosini nyota hao, kila mchezaji ndani ya Yanga ana umuhimu wake, kuwepo ndani ya kikosi kuna kitu kitaongeza na ukizingatia Aziz Ki ni kinara na mabao kwa sasa kuwepo kwake kunaendelea kumfanya kufunga na kufikia malengo, “ amesema Gamondi.
Ameongeza kuwa nyota hao wako sehemu ya mipango ya kuelekea mchezo wao wa keshokutwa dhidi ya KMC FC na wamejiandaa vizuri kukabiliana na mpinzani wake huyo licha ya kuwa wanaenda kucheza ugenini.
Gamondi amesema amesahihisha makosa yao ikiwemo safu ya ulinzi ambayo imeruhusu bao mbili katika michezo mitatu iliyopita, mechi ya kesho hataki kuona yanajirudia makosa haya.
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.