Serie A - UC Sampdoria v Inter Milan


Hakimiliki ya picha: Getty Images
 

2022/23 Italian Serie A

Matchday 22

UC Sampdoria v Inter Milan

Stadio Comunale Luigi Ferraris 
Genoa, Italy 
Monday, 13 February 2023 
Kick-off is at 21h45  
 
UC Sampdoria watakuwa mwenyeji wa Inter Milan katika mechi ya ligi kuu Italia Serie A ugani Stadio Comunale Luigi Ferraris Februari 13.
 
Matokeo ya hivi karibuni.
 
The Blue Circled, kama wanavyofahamika Sampdoria walipoteza 2-0 dhidi ya Atalanta BC ugenini Januari 28 na hawajapata ushindi katika mechi nne zilizopita za ligi.
 
Vile vile, Sampdoria hawajashinda mechi yoyote ya ligi katika mechi 10 zilizopita wakiwa nyumbani  ikiwa wameandikisha sare mbili na kupoteza mechi kumi ugani Stadio Comunale Luigi Ferraris.
 
Kwingineko, Inter wakiwa nyumbani walipata ushindi wa 1-0 dhidi ya mahasimu wa jadi AC Milan Februari 5 hivyo basi hawajapoteza mechi ya ligi katika michezo miwili iliyopita.
 
The Big Grass Snake, kama wanavyofahamika Inter Milan hawajapoteza mechi ya ligi katika michezo mitatu iliyopita wakiwa ugenini baada ya kuandikisha ushindi wa mechi mbili na sare moja.  
 
Athari za matokeo ya mechi hii.
 
Sampdoria wapo katika nafasi ya 19 katika msimamo wa ligi. Lengo lao ni kupunguza shinikizo la kushuka daraja kwa kupata ushindi dhidi ya Inter Milan.
 
Kwa upande mwingine, Inter wanafukuzia ubingwa wa ligi ya Serie A kwani wanashikilia nafasi ya pili kwenye jedwali, alama 13 nyuma ya viongozi wa ligi SSC Napoli. 
 
Inter chini ya mkufunzi Simone Inzaghi wanatarajia kupata ushindi dhidi ya Sampdoria huku wakiwa na matumaini Napoli watapoteza mechi yao dhidi ya US Cremonese Februari 12.
 
Habari za kikosi.
 
The Blue Circled ni miongoni mwa timu za ligi ya Serie A zilizo na majeruhi wengi; Manuel De Luca, Omar Colley, Abdelhamid Sabiri, Simone Trimboli, Andrea Conti na Ignacio Pussetto wote wakiuguza majeraha.
 
Inter Milan watakosa huduma za Dalbert na Joaquín Correa kwenye mechi hiyo kwani wanauguza kwa sasa.
 
Wachezaji muhimu
 
Manolo Gabbiadini amehusika katika magoli mengi zaidi kwa upande wa Sampdoria kuliko mchezaji mwingine yeyote kwenye mechi za ligi msimu huu kwani amefunga magoli mawili na kusaidia kupatikana goli moja.
 
Lautaro Martinez amekuwa mchezaji muhimu sana kwa upande wa Inter Milan kwani amefunga magoli 12 na kusaidia kupatikana kwa magoli matatu katika mechi za ligi.
 
Nukuu
 
"Tumekuwa na mchezo mzuri sana. Ni furaha kubwa kwangu kama mwalimu kushuhudia mchezo kama huu. Tumecheza vizuri sana. Pongezi kwa wachezaji ambao wameonyesha ushirikiano na kujituma zaidi,” Inzaghi alisema baada ya ushindi dhidi ya AC Milan.
 
"Tumeshinda dabi mbili kwa kipindi cha siku 20. Haikuwa rahisi kwa hivyo ni raha kubwa. Tuna matumaini makubwa katika mechi zijazo na tunatarajia wachezaji wote watakuwa wamepona. Tunatakiwa kuangalia maslahi yetu binafsi. Jumanne tulicheza mechi ngumu sana ya robo fainali dhidi ya Atalanta.
 
"Kipindi cha kwanza tulionyesha mchezo mzuri sana. Kipindi cha pili vile vile tulidhibiti mchezo vizuri. Tutafurahia ushindi huu kwa sasa. Mechi imekuja baada ya kuwa na mchezo mzuri kabisa dhidi ya Atalanta. Ni fahari kubwa kushinda dabi kwa mtindo huu.”
 
Takwimu baina ya timu hizi.
 
Inter walipata ushindi wa 3-0 dhidi ya Sampdoria walipokutana mara ya mwisho kwenye mechi ya ligi Oktoba 29 2022 ugani Stadio Giuseppe Meazza.
 
The Big Grass Snake hawajapoteza katika mechi nne za mwisho walizocheza na Blue Circled katika ligi ikiwa wameshinda mechi tatu na kupata sare moja.
 

Matokeo ya mechi tano za mwisho za ligi.

 
Mechi - 5
Sampdoria - 1
Inter - 3
Sare - 1
 

Ratiba ya mechi za Serie A mchezo wa 22.


Februari 10 Ijumaa

10:45pm - AC Milan v Torino FC

Februari 11 Jumapili

5:00pm - Empoli FC v Spezia Calcio
8:00pm - USA Lecce v AS Roma
10:45pm - SS Lazio v Atalanta BC

Februari 12 Jumapili

2:30pm - Udinese Calcio v US Sassuolo
5:00pm - Bologna FC v AC Monza
8:00pm - Juventus FC v ACF Fiorentina
10:45pm - SSC Napoli v US Cremonese

Februari 13 Jumatatu

8:30pm - Hellas Verona v US Salernitana
10:45pm - UC Sampdoria v Inter Milan
 

Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa​

Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.Chomoka na Odds


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 
 
 

Published: 02/08/2023