NBA - Dallas Mavericks v Los Angeles Lakers 


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022/23 National Basketball Association (NBA) season

Regular Season

Dallas Mavericks v Los Angeles Lakers 

American Airlines Center

Dallas, Texas, USA

Sunday, 26 February 2023 

23h30 

Dallas Mavericks na Los Angeles Lakers watamenyana kwenye ligi ya mpira wa kikapu National Basketball Association (NBA) mnamo Februari 26.

Takwimu baina ya timu hizi

Huu utakuwa mchezo wa 170 baina ya timu hizi kwenye mechi za NBA tangu msimu 1980/81 ambao ni msimu wa kwanza wa Mavericks NBA.

The Lakers wameshinda mechi 115 kati ya mechi hizo 169 ukilinganisha na ushindi wa mechi 54 kwa faida Mavericks. 

 

Mechi ya mwisho baina ya timu hizi.

Luka Doncic alionyesha mchezo mzuri sana Mavericks walipopata ushindi kwenye mechi ya mwisho baina ya timu hizi mbili mnamo Januari 13 2023. Mavericks waliibuka na ushindi wa 119-115 dhidi ya Lakers kwenye mechi hiyo.

Mechi hiyo iliandaliwa kwenye ukumbi wa Crypto.com Arena mjini Los Angeles. 

 

Athari ya matokeo ya mechi hiyo.

Ndoto ya the Mavericks kufuzu mechi za mchujo ipo wazi kwani wapo katika nafasi ya saba kwenye michezo ya Western Conference baada ya kushinda mechi 31 na kupoteza mechi 29.

Kwa upande wa Lakers, ndoto yao kushiriki mechi za mchujo ipo njia panda kwani wanashikilia nafasi ya 13 kwenye michezo ya Western Conference baada ya kushinda mechi 26 na kupoteza mechi 32. 

 

Wachezaji muhimu

Doncic aliyewabana sana Lakers walipokutana mwezi Januari atakuwa na nia ya kuwazamisha zaidi mabingwa hao wa zamani wa NBA kwa mara nyingine watakapokutana tena.

LeBron James ndiye mchezaji nyota wa timu ya Lakers na alionyesha weledi wake kwenye mechi ya kwanza baina ya timu hizi. Lakers wana matarajio makubwa kuwa ndiye mchezaji atakaye wasaidia kupata ushindi na kuokoa msimu wao japo kwa sasa.

 

Nukuu

"Hatuna muda na hatuwezi kuendelea kupoteza mechi zaidi,” alisema kocha wa Lakers Darvin Ham hivi majuzi akisisitiza umuhimu wa kushinda mechi zilizosalia.

"Tunastahili kutambua kuwa bado tupo katika nafasi ambayo tunaweza kubadilisha mwelekeo wetu msimu huu. Tunatakiwa kuongeza juhudi. Hakuna muda wa kuongeza. Ni muda wa vitendo.

"Tutachukua maarifa kutoka mechi tulizoshinda na tulizopoteza hadi kufikia sasa. Bado tuna uwezo na nafasi ya kutia juhudi na kufuzu mechi za mchujo.”
 

Ratiba ya mechi za NBA – tarehe 25 na 26 Februari


Februari 25 Jumamosi

03:00am - Washington Wizards v New York Knicks
03:30am - Atlanta Hawks v Cleveland Cavaliers
03:30am - Milwaukee Bucks v Miami Heat
04:00am - Chicago Bulls v Brooklyn Nets
04:00am - Minnesota Timberwolves v Charlotte Hornets
06:00am - Golden State Warriors v Houston Rockets
06:00am v Phoenix Suns v Oklahoma City Thunder
06:30am - Los Angeles Clippers v Sacramento Kings
8:00pm - Detroit Pistons v Toronto Raptors

Februari 26 Jumapili

03:00am - Charlotte Hornets v Miami Heat
03:00am - Orlando Magic v Indiana Pacers
03:30am - New York Knicks v New Orleans Pelicans
04:00am - Memphis Grizzlies v Denver Nuggets
04:30am - Philadelphia 76ers v Boston Celtics
05:00am - Utah Jazz v San Antonio Spurs
9:00pm - Milwaukee Bucks v Phoenix Suns
11:00pm - Atlanta Hawks v Brooklyn Nets
11:30pm - Chicago Bulls v Washington Wizards
11:30pm - Dallas Mavericks v Los Angeles Lakers
 

Bashiri Mpira wa Kikapu na Betway


Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni mpira wa miguu, mpira wa kikapu, rugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.




Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.

Published: 02/24/2023