Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022/23 Spanish La Liga
Matchday 22
Atletico Madrid v Athletic Bilbao
Estádio Cívitas Metropolitano
Madrid, Spain
Sunday, 19 February 2023
Kick-off is at 19h30
Atletico Madrid itakuwa mwenyeji wa Athletic Bilbao katika
mechi ya ligi ugani Estádio Cívitas Metropolitano Februari 19.
Hali yao ya sasa
Atletico Madrid maarufu kama The Mattress Makers walipata ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya Celta Vigo Februari 12 na kufikisha msururu wa mechi tano za ligi bila kupoteza.
Vile vile, Atletico hawajapoteza mechi mbili za ligi zilizopita wakiwa nyumbani huku wakiandikisha sare moja na ushindi mmoja ugani Estádio Cívitas Metropolitano.
Bilbao walipata ushindi wa 2-1 ugenini dhidi ya Valencia CF Februari 11 na hawajapoteza katika mechi mbili za ligi zilizopita.
Ushindi dhidi ya Valencia ulifikisha kikomo msururu wa mechi saba ugenini bila kushinda kwani walikuwa wameandikisha sare tatu na kupoteza mechi nne.
Athari ya matokeo ya mechi hii.
Atletico wanashikilia nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi huku lengo lao likiwa kusalia katika nafasi hiyo au bora ligi ikikamilika.
Timu ya Diego Simeone inalenga kupata ushindi dhidi ya Bilbao ambao wanaonekana kuimarika na kutafuta nafasi ya nne msimu utakapofika kikomo.
Bilbao wapo katika nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi ikiwa ni alama sita nyuma ya Atletico na ushindi wa mechi hii utapiga jeki azma yao ya kumaliza katika nafasi ya nne.
Vikosi
Atletico hawana majeruhi kuelekea mchezo huo ila watakosa huduma za mlinzi Stefan Savic aliyeonyeshwa kadi nyekundu kwenye mchezo dhidi ya Celta Vigo.
Hata hivyo, Bilbao wana hofu na hali ya mchezaji Ander Herrera na Íñigo Martínez ambao kuna uwezekano watakosa mechi hiyo kutokana na majeraha tofauti.
Wachezaji muhimu
Baada ya kufunga goli lake la kwanza kwa faida ya Atletico dhidi ya Celta Vigo, Memphis Depay atakuwa na uchu wa kufunga magoli zaidi dhidi ya Bilbao.
Kwa upande wa Bilbao, matumaini yao yatakuwa kwa mchezaji Ohian Sancet ambaye hadi kufikia sasa amefunga magoli 8 kwenye mechi 19 za ligi kuwapa ushindi dhidi ya Atletico.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Nukuu
"Mechi ilikuwa ya ajabu kama tulivyoitarajia,” alisema meneja wa Bilbao Ernesto Valverde baada ya ushindi dhidi ya Valencia.
"Tulifahamu wapinzani wetu wapo chini ya shinikizo kubwa kutokana na matokeo yao ya hivi karibuni na mambo mengine kuhusu mchezo huu.
"Tulifuata mbinu na kupata alama zote tatu. Ni ushindi muhimu katika kipindi hiki cha msimu ambapo timu zinaonekana kutoshana nguvu,” aliendelea.
"Tutafurahia ushindi huu. Kwenye mechi ya kombe la Copa haikuwa changamoto sana lakini mechi ya leo ilikuwa ngumu kidogo. Tulilazimika kujituma zaidi.”
Matokeo baina ya timu hizi
Atletico waliibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Bilbao walipokutana mara ya mwisho kwenye mechi ya ligi mnamo Oktoba 15 2022 ugani San Mames Barria.
Ushindi huo ulifikisha kikomo msururu wa mechi tatu bila ushindi kwa upande wa Atletico dhidi ya Bilbao kwenye ligi baada ya kuandikisha sare mbili na kupoteza mechi moja kabla ya mechi hiyo ya Oktoba.
Takwimu baina ya timu hizi mechi 5 za mwisho za ligi.
Mechi - 5
Atletico - 2
Bilbao - 2
Sare - 1
Ratiba ya mechi za La Liga mchezo wa 22.
Februari 17 Ijumaa
11:00pm- Girona FC v UD Almeria
Februari 18 Jumamosi
4:00pm - Real Sociedad v Celta Vigo
6:15pm - Real Betis v Real Valladolid
8:30pm - Real Mallorca v Villarreal
11:00pm- CA Osasuna v Real Madrid
Februari 19 Jumapili
4:00pm - Elche CF v RCD Espanyol
6:15pm - Rayo Vallecano v Sevilla FC
8:30pm - Atletico Madrid v Athletic Bilbao
11:00pm- FC Barcelona v Cadiz CF
Februari 20 Jumatatu
11:00pm - Getafe CF v Valencia CF
Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa
Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.