Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022/23 Spanish La Liga
Matchday 23
Real Madrid v Atletico Madrid
Estadio Santiago Bernabéu
Madrid, Spain
Saturday, 25 February 2023
Kick-off is at 19h30
Real Madrid watakutana na watani wao Atletico Madrid kwenye
mechi ya ligi kuu Uhispania mnamo Februari 25 ugani Estadio Santiago Bernabéu.
Hali yao kwa sasa.
The Whites ambao ni Real Madrid walipata ushindi wa 2-0 ugenini dhidi ya CA Osasuna Februari 18 na hawajapoteza mechi katika michezo miwili ya ligi iliyopita.
Vile vile, Real Madrid hawajapoteza mchezo wa ligi katika mechi 14 za mwisho wakiwa nyumbani kwani wameandikisha sare nne na kushinda mechi 10 uwanjani Estadio Santiago Bernabéu.
Atletico waliibuka na ushindi wa 1-0 nyumbani dhidi ya Athletic Bilbao Februari 19 na kufikisha msururu wa mechi sita kwenye ligi bila kushindwa.
Atletico Madrid maarufu kama the Mattress Makers hawajapoteza mechi katika michezo mitatu ya mwisho wakiwa ugenini baada ya kuandikisha sare moja na kushinda mechi mbili.
Athari za matokeo ya mechi hii.
Madrid wanashikilia nafasi ya pili kwenye jedwali la ligi na alama nane nyuma ya viongozi Barcelona hivyo basi watafanya kila juhudi kuhakikisha ushindi.
Madrid ambao ni mabingwa watetezi wa ligi hiyo wana imani watashinda mechi hiyo na kutarajia Barcelona watapoteza mechi yao dhidi ya UD Almeria Februari 26.
Atletico Madrid wanashikilia nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi na ushindi kwenye mechi dhidi ya Real utapiga jeki azma yao ya kumaliza nne bora.
Vikosi
Toni Kroos amerudi mazoezini kuelekea mechi dhidi ya Atletico baada ya kukosa mechi dhidi ya Osasuna kutokana na jeraha. Mchezaji mwenza Ferland Mendy atazidi kuuguza jeraha lake.
Kwa upande mwingine, Atletico Madrid wana majeruhi mmoja tu kwa sasa ambaye ni Thomas Lemar kuelekea mechi hiyo.
Wachezaji muhimu
Meneja wa Madrid Carlo Ancelotti kwa mara nyingine matumaini yake yatakuwa kwa mchezaji Vinicius Junior ambaye alisaidia goli lake la nne la msimu walipocheza dhidi ya Osasuna.
Atletico wanatarajia umahiri wa Antoine Griezmann aliyewapa ushindi dhidi ya Bilbao utawawezesha ushindi kwenye dabi.
Nukuu
"Mechi hii ilikuwa na ushindani mkali baina ya timu zote na zilionyesha mchezo wa kufurahisha,” Ancelotti alisema baada ya mechi dhidi ya Osasuna.
"Tumefurahishwa jinsi timu ilivyocheza. Wameonyesha mchezo mzuri sana. Mechi haikuwa rahisi lakini walifahamu wakati mwafaka na kufunga magoli. Tumeridhiswa na hali hiyo. Tunasubiri mechi dhidi ya Liverpool ugani Anfield Februari 21 tukiwa katika hali nzuri.
"Aurelien Tchouameni alikuwa na maumivu ya tumbo. Nahisi Karim Benzima atakuwa tayari kucheza mechi hiyo na Toni Kroos amerejea mazoezini. Dani Carvajal vile vile atashiriki mechi hiyo ugani Anfield."
Takwimu baina ya timu hizi.
Real Madrid waliibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Atletico walipokutana mara ya mwisho kwenye ligi ugani Estádio Cívitas Metropolitano Septemba 18 2022.
Huu ulikuwa ni ushindi wa pili wa Real dhidi ya Atletico katika mechi tatu za ligi zilizopita huku Atletico wakishinda mchezo wa tatu mnamo Mei 2022.
Takwimu baina ya timu hizi, mechi 5 za mwisho za ligi.
Mechi - 5
Real - 3
Atletico - 1
Sare - 1
Ratiba ya mechi za La Liga mchezo wa 23.
Februari 24 Ijumaa
10:00pm - Elche CF v Real Betis
Februari 25 Jumamosi
3:00pm - RCD Espanyol v Real Mallorca
5:15pm - Cadiz CF v Rayo Vallecano
7:30pm - Real Madrid v Atletico Madrid
10:00pm - Valencia CF v Real Sociedad
Februari 26 Jumapili
3:00pm - Athletic Bilbao v Girona FC
5:15pm - Celta Vigo v Real Valladolid
7:30pm - UD Almeria v FC Barcelona
10:00pm - Sevilla FC v CA Osasuna
Februari 27 Jumatatu
10:00pm - Villarreal CF v Getafe CF
Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa
Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.