EPL - Tottenham Hotspur v Chelsea


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022/23 English Premier League

Matchday 25

Tottenham Hotspur v Chelsea

Tottenham Hotspur Stadium
London, England
Sunday, 26 February 2023
Kick-off is at 15h30  
 
Tottenham wanatarajia kupata ushindi wa nne katika mechi tano za ligi watakapoialika Chelsea ugani Tottenham Hotspur Stadium Jumapili Februari 26.
 
Spurs walipata ushindi wa 2-0 dhidi ya West Ham Jumapili iliyopita baada ya kopoteza 4-1 dhidi ya Leicester hapo awali kwenye mechi ya ligi.
 
Kabla ya kupoteza mechi dhidi Leicester King Power Stadium mnamo Februari 11, vijana wa Antonio Conte walikuwa wamepata ushindi wa 1-0 mechi mbili mfululizo; dhidi ya Fulham na Manchester City.
 
Timu hiyo kutoka Kaskazini mwa London inachukua nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi nyuma ya Manchester United na alama 7 na alama 12 nyuma ya viongozi wa ligi Arsenal ambao waliibuka na ushindi wa 4-2 dhidi ya Aston Villa.
 
Newcastle walishuka hadi nafasi ya tano baada ya kupoteza 2-0 dhidi ya Liverpool na ambayo ilikuwa ni mechi yao ya nne ya ligi bila ushindi.

Kai Havertz
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Kiwango cha Chelsea pia kimedidimia katika mechi za hivi karibuni. Katika mechi yao ya mwisho ya ligi, Chelsea walichapwa 1-0 na Southampton ambao wanavuta mkia. Hii ilikuwa mechi ya nne ya Chelsea bila ushindi.
 
Kufuatia matokeo hayo, timu hiyo chini ya Graham Potter imeandikisha ushindi katika mechi mbili tu tangu ligi iliporejea baada ya kombe la dunia mwezi Desemba.
 
Matokeo hayo yamepelekea Chelsea kushuka kwenye msimamo wa ligi na sasa wapo katika nafasi ya 10 nyuma ya Brentford (9), Liverpool (8) na Brighton (7) mtawalia wote wakiwa na alama 35.
 
Chelsea wapo nyuma ya timu hizo tatu na alama 4 na alama 3 mbele ya Aston Villa wanaoshikilia nafasi ya 11. Crystal Palace, Nottingham Forest na Leicester wanashikilia nafasi ya 12, 13 na 14 mtawalia. 
 
The Blues wamekuwa na uhaba wa mabao msimu huu ikiwa wamefunga magoli 23 tu katika mechi 23 za ligi. Kai Havertz ndiye mfungaji bora wa kikosi hicho akiwa na magoli matano tu na akiwa hajafunga bao katika mechi nne za mwisho za ligi. Sajili mpya Joao Felix alifunga goli dhidi ya the Hammers na Potter anatarajia mchezaji huyo wa Ureno atasaidia kutatua ubutu wao kwenye safu ya ushambuliaji.

Harry Kane
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Kwa upande wa Spurs, Harry Kane anazidi kuonyesha makali yake kwenye lango ikiwa amefunga magoli 17 kwenye mechi 23 za ligi na kusawazisha idadi yake ya msimu uliopita. Hivi majuzi, mshambuliaji huyo mwenye miaka 29 alivunja rekodi ya mfungaji bora wa klabu hiyo iliyoshikiliwa na Jimmy Greaves kwa kufunga goli la 267.
 
Kwenye habari ya vikosi, Yves Bissouma (kisigino), Hugo Lloris (goti), Ryan Sessegnon (paja) and Rodrigo Bentancur (goti) wa Tottenham watakosa mechi hiyo. Potter atawakosa wachezaji kadhaa wa kikosi cha kwanza; Armando Broja na Christian Pulisic (goti), N'Golo Kante (paja), Cesar Azpilicueta (kichwa) na Edouard Mendy (mkono).
 
Kocha msaidizi wa Conte, Cristian Stellini alizungumzia umuhimu wa kucheza na wachezaji wa pembeni katika mechi kwa sababu wanasaidi wachezaji kama vile Dejan Kulusevski na Son Heung-Min kuwa na uhuru zaidi.
 
"Kutumia wachezaji wa pembeni katika mechi na kufunga magoli mengi ni moja ya malengo yetu na maagizo tunayowapa wachezaji,” Stellini aliambia SPURSPLAY.
 
"Wachezaji hao wanasaidia kutengeneza nafasi zaidi kwa ajili ya wachezaji Dejan Kulusevski na Sonny.
 
"Sharti tuwe na muendelezo wa wa matokeo mazuri kwa sababu tumeingia nne bora na tunahitaji kucheza kama tulivyocheza leo ili kusalia tulipo.”
 
Potter anakiri kuwa timu yake haipo katika wakati mzuri. Majeruhi wanazidi kuongeza na vile vile anajaribu kutafuta mbinu za kutengeneza kikosi na kuwaleta wachezaji wapya kwenye kikosi.
 
"Hii ndio hali yetu kwa sasa. Kuwaunganisha wachezaji wapya kwenye kikosi kunachukua muda na pia kunachangia kwa kiasi fulani matokeo yetu. Tunapoteza mechi na inaeleweka,” alisema.
 
"Jukumu langu ni kusaidia timu hii wakati wa kipindi hiki kigumu na jambo hili nalielewa.
 
"Majeruhi wamekuwa wengi. Sio jambo geni hilo katika ligi ya Premier. Hizi changamoto zipo lakini sio sababu unapopoteza mechi.”
 

Takwimu baina ya timu hizi, mechi 5 za mwisho za ligi.

Mechi - 5
Tottenham - 0
Chelsea - 3
Sare - 2
 

Ratiba ya mechi za Premier mchezo wa 25.

 
Februari 24 Ijumaa
 
11:00pm: Fulham v Wolverhampton Wanderers
 
Februari 25 Jumamosi
 
6:00pm: Everton v Aston Villa
 
6:00pm: Leeds United v Southampton
 
6:00pm: Leicester City v Arsenal
 
6:00pm: West Ham United v Nottingham Forest
 
8:30pm: Bournemouth v Manchester City
 
10:45pm: Crystal Palace v Liverpool
 
Februari 26 Jumapili
 
4:30pm: Tottenham Hotspur v Chelsea
 

Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa​

Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.Chomoka na Odds


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 
 

Published: 02/24/2023