Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022/23 English Premier League
Matchday 24
Manchester United v Leicester City
Old Trafford
Manchester, England
Sunday, 19 February 2023
Kick-off is at 16h00
Manchester United wanatazamia kuendeleza azma yao ya kushinda taji la
ligi watakapowakaribisha Leicester City ugani Old Trafford Jumapili Februari 19.
Kwa sasa The Red Devils wapo alama tano nyuma ya viongozi wa ligi Arsenal baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Leeds uwanjani Elland Road Jumapili iliyopita huku mechi ya kwanza baina ya timu hizo ikimalizika sare ya 2-2 siku mbili kabla.
Vijana wa Erik ten Hag hawajapoteza mechi ya ligi katika mechi tatu zilizopita tangu walipochapwa na Arsenal 3-2 the Emirates Stadium Januari 22 na wapo nafasi ya tatu alama mbili ya mahasimu wao City ambao watakutana na Arsenal katikati mwa juma.
Newcastle wapo alama tano nyuma ya United baada ya kuandikisha sare ya tatu mfululizo ambayo ni sare ya 11 msimu huu na kushika nafasi ya nne huku Tottenham wakishikilia nafasi ya tano alama mbili nyuma ya Newcastle.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
The Foxes walipata ushindi wa 4-1 dhidi ya Spurs King Power Stadium Jumapili iliyopita baada ya kutoka goli moja chini na kufunga magoli matatu kipindi cha kwanza kabla ya kufunga goli la nne dakika za mwisho za mchezo.
Leicester chini ya Brandon Rodgers ilipitia kipindi kigumu cha matokeo mseto mwezi wa Desemba na Januari baada ya kucheza mechi tano bila ushindi kabla ya kuandikisha ushindi mfululizo mwezi huu.
Timu ya Leicester kwa sasa ipo alama sita juu ya kiwango cha kushushwa daraja katika nafasi ya 13. Hii ni alama tano nyuma ya timu inayoshikilia nafasi ya 10. Chelsea wanashika nafasi ya 9, alama saba juu ya Leicester.
Mchezo wa Bruno Fernandes wa United unaonekana kuimarika kwa sasa kwani amefunga magoli matano na kuchangia manne katika mechi 22 za ligi msimu huu. Mchezaji huyo raia wa Ureno amepewa jukumu la kuwa nahodha anapokosekana nahodha rasmi Harry Maguire.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
James Maddson amekuwa mchezaji nyota na muhimu kwa upande wa Leicester msimu huu huduma zake zilikosekana sana mwezi uliopita baada ya kupata jeraha la goti na kukaa nje mechi nne. Kiungo huyo mshambuliaji alifunga goli moja na kusaidia kupatikana goli moja dhidi ya Tottenham. Kwa sasa idadi yake kwenye ligi imefikia magoli tisa.
Kwenye habari za vikosi, wenyeji United watakosa huduma za Donny van de Beek (goti) na Christian Eriksen (kifundo cha mguu), huku Casemiro akimalizia marufuku yake ya mechi mbili. Kuna nafasi kubwa Scott McTominay, Anthony Martial (kinena) na Antony (mguu) watarejea uwanjani mwezi huu.
James Justin (mguu) atakuwa nje msimu mzima kwa upande wa Leicester na Ryan Bertrand (goti) atakuwa nje kwa angalau mwezi mmoja. Jonny Evans, Youri Tielemans (wote wauguza jeraha la mguu) na Boubakary Soumare (paja) wanaweza kurejea uwanjani wiki mbili zijazo.
Ten Hag alisifia uchezaji wa mshambuliaji Marcus Rashford ambaye alifunga katika mechi zote mbili dhidi ya Leeds wiki iliyopita akimtaja kuwa mmoja wa washambuliaji bora ulaya.
"Bilas haka ni mmoja wao,” alisemaTen Hag. "Nilishawishiwa na uwezo tangu mwanzo. Nilitamani sana kufanya kazi naye. Nilijua naweza kumsaidia zaidi.
"Anaelewa mbinu, ana uwezo mkubwa na ana uwezo wa kuimarika zaidi. Akizidi kujituma atafunga magoli zaidi kwa sababu anaweza kufunga kupitia mguu wa kulia, kushoto na pia kichwa.”
Rodgers alivutiwa na kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wake dhidi ya Spurs na hana shaka kuwa timu yake ina uwezo wa kukabiliana na timu bora katika ligi wakizidi kuonyesha ari hiyo.
"Sio kisingizio ila kuna sababu ya sisi kuwa tulipo na hatukuweza kununua wachezaji hadi dirisha doro la uhamisho la Januari,” alisema Rodgers.
"Tumeimarika sana. Jinsi tunavyocheza mchezo wetu na uchu wa kupata matokeo mazuri. Tunataka kucheza kwa kasi na mchezo wa kuvutia. Tunacheza vizuri na kupata matokeo ya kuridhisha.
"Muda wote nimekuwa nikisema wachezaji hawa wana uwezo. Baada ya kufungwa goli la mapema walijituma vilivyo na kushinda mchezo.”
Matokeo baina ya timu hizi katika mechi 5 za ligi zilizopita.
Mechi - 5
Man United - 1
Leicester - 2
Sare - 2
Ratiba ya mechi za ligi ya Premier mchezo wa 24.
Februari 18 Jumamosi
2:30pm: Aston Villa v Arsenal
5:00pm: Brentford v Crystal Palace
5:00pm: Brighton & Hove Albion v Fulham
5:00pm: Chelsea v Southampton
5:00pm: Everton v Leeds United
5:00pm: Nottingham Forest v Manchester City
5:00pm: Wolverhampton Wanderers v Bournemouth
7:30pm: Newcastle United v Liverpool
Februari 19 Jumapili
4:00pm: Manchester United v Leicester City
6:30pm: Tottenham Hotspur v West Ham United
Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa​
Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.