EPL - Liverpool v Everton


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022/23 English Premier League

Matchday 23

Liverpool v Everton

Anfield
Liverpool, England
Monday, 13 February 2023
Kick-off is at 22h00  
 
Everton wana nafasi kubwa ya kupata ushindi dhidi ya Liverpool katika dabi ya 242 ya Merseyside watakapokutana kwenye mechi ya ligi ugani Anfield Jumatatu Februari 13.
 
The Toffees wamekuwa na msimu wa kusahau na matokeo mabaya ambayo yalipelekea Frank Lampard kupoteza kazi kama kocha wa timu hiyo Januari 23 baada ya kupoteza 2-0 dhidi ya West Ham United, ikiwa ni mechi ya tatu kupoteza mfululizo.
 
Lampard alifutwa kazi timu hiyo ikiwa na alama 15 sawia na Southampton wakishikilia nafasi ya mwisho kwenye ligi. Baada ya kutwaa kibarua cha kuinoa timu hiyo, Sean Dyche ameanza vizuri kwa kupata ushindi wa 1-0 dhidi ya Arsenal ambao wanaongoza ligi mnamo Februari 4.
 
Matokeo hayo yalifikisha kikomo msururu wa mechi nane bila ushindi kwa Everton na sasa wapo katika nafasi ya 18, alama tatu nyuma ya Leicester walio katika nafasi ya 14.

Mo Salah
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Kwa wapinzani wao siku hiyo, Liverpool wamekuwa na matokeo ya kutamausha msimu huu na sasa wapo alama 21 nyuma ya viongozi Arsenal wakiwa katika nafasi ya 10.
 
Vijana wa Jurgen Klopp walipoteza mechi dhidi ya Wolves 3-0 Februari 4, ambayo ilikuwa ya tatu kupoteza katika mechi nne zilizopita na kuwaacha bila ushindi wowote mwaka huu.
 
The Toffees wameshinda mechi mbili tu za dabi katika michezo 25 ya ligi iliyopita dhidi ya majirani wao na sasa watakuwa na imani kupata ushindi watakapokutana wakati huu.
 
Liverpool wanatarajia mshambuliaji wao Mohamed Salah atawasaidia kupata ushindi licha ya kuwa amekuwa na wakati mgumu na hajaonyesha makali yaliyomfanya kushinda taji la mfungaji bora kwa pamoja na Son Hueng-Min wa Tottenham msimu uliopita.
 
Salah amefunga magoli saba tu katika mechi ishirini za ligi ambayo ni idadi ndogo sana ukulinganisha na magoli 23 ya msimu 2021-22 aliyofunga na kusaidia Liverpool kumaliza katika nafasi ya pili katika ligi.  

Demarai Gray of Everton
Hakimiliki ya picha: Getty Images

 
Everton wamekuwa wakikosa huduma za mshambuliaji Dominic Calvert-Lewin ambaye amekuwa na majeraha ya mara kwa mara kipindi cha misimu miwili iliyopita. Washambuliaji wengine wa kikosi hicho hawajaweza kuziba pengo lake huku mfungaji wao bora katika ligi akiwa Demarai Gray na idadi ya magoli matatu.
 
Alex Iwobi amekuwa mchezaji nyota wa timu hiyo huku akifunga goli moja na kuchangia magoli sita kwenye mechi 21. Inakisiwa atakuwa mchezaji muhimu kufungua safu wa ulinzi watakapocheza dhidi ya Liverpool.
 
Katika habari za kikosi, wenyeji Liverpool watakuwa bila wachezaji wa safu ya ulinzi Virgil van Dijk na Ibrahima Konate wanaouguza majeraha ya paja, mshambuliaji Roberto Firmino ambaye anatarajiwa kupona baada ya muda usio mrefu na Diogo Jota anatarajiwa kuanza mazoezi wiki ijayo. Vile vile Liverpool watakosa huduma za Luiz Diaz anayeuguza jeraha la goti, Arthur Melo jeraha la paja na Fabio Tavares ambaye ni mgonjwa.
 
Kwa upande wa Everton, wachezaji Calvert-Lewin akiwa na jeraha la paja na Michael Keane aliye na jehara ya goti huenda watakosa mechi hiyo. Mchezaji james Garner (mgongo), Andros Townsend na Nathan Patterson ambao wote wanauguza majeraha ya goti watakosa mechi hiyo pia.
 
Klopp amekiri kuwa wachezaji wake wanakosa hali ya kujiamini baada ya matokeo ya hivi karibuni ila anataka kuona juhudi zaidi kutoka kwao.
 
"Ni vigumu kuelezea hali yetu tangu mwaka huu kuanza. Timu hii haijiamini tena. Hilo ni wazi. Dakika za kwanza 12 zilionyesha wazi. Safu ya ulinzi haikuwa imara, hatukucheza kwa kushirikiana vizuri na kasi yetu ilikuwa chini,” alisema raia huyo wa Ujerumani.
 
"Tunahitaji kuzuia mashambulizi vizuri na kudhibiti uchezaji wa wapinzani wetu. Mambo kama haya tu.”
 
Mkufunzi wa Everton Sean Dyche anatarajia ushindi dhidi ya the Gunners motisha zaidi huku akiwakumbusha wachezaji wake kuhusu kazi kubwa ilioko mbele yao wiki zijazo.
 
"Nimewaambia kuwa huu uwe mwanzo mpya. Tunaweka misingi ya vitu tunavyotaka kufanikisha kama kundi na huu ni mwanzo. Haijalishi utapata ushindi dhidi ya timu gani,” alisema.
 
"Ushindi huu haujatatua tatizo lolote. Tunatakiwa kushinda zaidi na zaidi baada ya matoke ohayo ila ni mwanzo mwafaka. Kwa sasa Arsenal wanacheza vizuri na wanapata matokeo mazuri ila ushindi wa mechi ifuatayo hauna uhakika kisa tulishinda Arsenal. Nimewaeleza wachezaji wangu hilo tayari.
 
"Nimewaeleza kuwa Jumatatu tunaanza upya. Kuendeleza na kazi na kujiimarisha zaidi.”
 

Matokeo baina ya timu hizi, mechi tano za mwisho za ligi.

Mechi - 5
Liverpool - 2
Everton - 1
Sare- 2
 

Ratiba ya mechi za ligi Premier mchezo wa 23.

 
Februari 11 Jumamosi
 
2:30pm: West Ham United v Chelsea
 
5:00pm: Arsenal v Brentford
 
5:00pm: Crystal Palace v Brighton & Hove Albion
 
5:00pm: Fulham v Nottingham Forest
 
5:00pm: Leicester City v Tottenham Hotspur
 
5:00pm: Southampton v Wolverhampton Wanderers
 
7:30pm: Bournemouth v Newcastle United
 
Februari 12 Jumapili
 
4:00pm: Leeds United v Manchester United
 
6:30pm: Manchester City v Aston Villa
 
Februari 13 Jumatatu
 
10:00pm: Liverpool v Everton
 

Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa​

Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.Chomoka na Odds


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 
 

Published: 02/08/2023