City na Spurs kutibua vumbi, mechi ya ligi


Hakimiliki ya picha: Getty Images
 


2022/23 English Premier League

Matchday 22

Tottenham Hotspur v Manchester City

Tottenham Hotspur Stadium
London, England
Sunday, 5 February 2023
Kick-off is at 19h30  
 
Manchester City wanatazamia kuendeleza shinikizo kwa viongozi wa ligi Arsenal watakapo safari kucheza na Tottenham Jumapili Februari 5.
 
The Citizens walihakikisha wanazidi kuwa alama tano nyuma za Arsenal kwa kuwashinda 3-0 Wolves mnamo Januari 22, mabao yaliyofungwa na Erling Haaland ambaye sasa amefikisha idadi ya mabao 25 ya ligi.
 
Pep Guardiola na vijana wake walicheza dhidi ya Spurs Januari 19 ambapo walilazimika kutoka nyuma mabao mawili na kupata ushindi wa 4-2 ugani Etihad Stadium.

John Stones
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
  
City watakosa huduma za mchezaji John Stones kwenye mechi hiyo ugani Tottenham Hotspur Stadium baada ya mlinzi huyo kupata jeraha kwenye mechi ya FA dhidi ya Arsenal Januari 27 ambapo City walipata ushindi wa 1-0.
 
"Hakuwa tayari leo baada ya kumtazama dakika za kwanza za mchezo. Pengine alikuwa na uchovu. Katika hali hiyo ni rahisi kupata jeraha,” alikiri Guardiola.
 
Tottenham walipata ushindi wa 1-0 dhidi ya Fulham Januari 23 baada ya mechi mbili za ligi bila ushindi na sasa wapo katika nafasi ya tano.
 
Tottenham imekuwa ikiwapa City wakati mgumu mara nyingi wanapokutana ikiwa wameshinda mechi nne katika mechi 10 zilizopita katika mashindano yote, pamoja na mechi ya nusu fainali ya UEFA mwaka 2019.
 
Antonio Conte amesisitiza umuhimu wa kutoruhusu magoli ikiwa ni mechi sita tu za msimu ambazo hawajaruhusu goli, baada ya kuruhusu magoli sita dhidi ya Arsenal na City kwa pamoja kabla ya mchezo dhidi ya Fulham, Craven Cottage.

Harry Kane
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
"Ni muhimu kumaliza mchezo bila kuruhu goli hasa kwa Hugp Lloris na pia timu nzima,” Conte aliambia SPURSPLAY baada ya mechi dhidi ya Fulham.
 
"Kama nilivyosema baada ya mchezo uliopita dhidi ya City, ilikuwa jambo la kushangaza kwa maoni yangu kuruhusu magoli 21 katika mechi 10 zilizopita ambalo sio jambo la kawaida kwa timu zangu. sio kawaida kwa Tottenham. Safu ya ushambuliaji ikiwa imara lakini safu ya ulinzi inaruhusu kiholela, mabadiliko yanahitajika kwa kweli.  
 
"Lazima tuanze upya kutoka hapa. Zimesalia mechi 17 msimu huu kukamilika na sharti tujitume vilivyo kisha tutaona tutafikia wapi kwenye jedwali.”
 

Takwimu baina ya timu hizi, mechi tano za mwisho za ligi.

Mechi - 5
Tottenham - 3
Man City - 2
Sare - 0
 

Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa​

Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.Chomoka na Odds


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.


 
 
 
 
 

Published: 02/01/2023