Barcelona na Sevilla kumenyana kwenye mechi ya La liga


Image copyright: Getty Images

 

2022/23 Spanish La Liga

Matchday 20

FC Barcelona v Sevilla FC 

Spotify Camp Nou
Barcelona, Spain 
Sunday, 5 February 2023
Kick-off is at 23h00  
 
FC Barcelona wataalika Sevilla FC ugani Spotify Camp Nou kwa ajili ya mechi ya ligi mnamo Februari 5.
 
Barca walipata ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya Girona FC katika mechi yao ya ligi ya mwisho ya Januari 28.
 
Barcelona hawajapoteza mechi ya ligi katika mechi tisa za mwisho huku wakiandikisha ushindi mara nane mfululizo na kupata sare moja.

Xavi
Image copyright: Getty Images
 
 
Vile vile, Barca hawajapoteza mechi yoyote ya ligi katika mechi tisa zilizopita wakiwa nyumbani baada ya kuandikisha ushindi mara saba na sare mbili ugani Spotify Camp Nou.
 
“Nimefurahishwa na ushindi huu. Haukuwa rahisi lakini pia tunahitaji kujitathmini. Hatukutengeneza nafasi nyingi kama kawaida yetu,” alisema meneja wa Barca Xavi Hernandez baada ya ushindi dhidi ya Girona.
 
“Tulimudu mchezo vizuri tulipomiliki mpira. Tunapiga pasi nzuri ila pasi ya mwisho inakosa nia. Girona walitupa nafasi ya kumiliki mpira wakati mwingi hivyo basi tukajisahahu kabisa na kijiondoa kwenye mbinu zetu hadi mwisho wa mchezo.
 
“Tumepiga hatua kubwa tangu msimu jana. Kuna mambo mengi ya kufanyia kazi ila nafurahishwa na hatua tuliyopiga.”

Kwingineko, walipata ushindi mnono wa 3-0 nyumbani dhidi ya Elche CF katika mchezo uliopita wa ligi uliochezwa Januari 28.
 
Kwa sasa, Sevilla hawajapoteza mchezo wa ligi katika mechi mbili zilizopita huku wakiandikisha ushindi mara mbili mfululizo.
 
Hata hivyo, Sevilla hawajashinda mechi ya ligi katika mechi nne zilizopita wakiwa ugenini baada ya kuandikisha sare mbili mfululizo na kupoteza mechi mbili.
 
Mechi ya mwisho ya ligi baina ya Barcelona na Sevilla ilichezwa mamo Septemba 3 2022.
 
Barcelona waliibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya Sevilla katika mechi hiyo iliyochezewa Estadio Ramón Sánchez Pizjuán uwanja uliopewa jina hilo kwa heshima za rais wa klabu hiyo wa zamani Ramón Sánchez-Pizjuán.
 

Takwimu baina ya timu hizi, mechi tano za mwisho za ligi.

Mechi - 5
Barcelona - 3
Sevilla - 0
Sare - 2
 

Ratiba ya mechi za La Liga mchezo wa 20.


Februari 3 Ijumaa

11:00pm - Athletic Bilbao v Cadiz CF

Februari 4 Jumamosi

4:00pm - RCD Espanyol v CA Osasuna
6:15pm - Elche CF v Villarreal CF
8:30pm - Atlético Madrid v Getafe CF
11:00pm - Real Betis v Celta Vigo

Februari 5 Jumapili

4:00pm - Real Mallorca v Real Madrid
6:15pm - Girona FC v Valencia CF
8:30pm - Real Sociedad v Real Valladolid
11:00 - FC Barcelona v Sevilla FC

Februari 6 Jumatatu

11:00pm - Rayo Vallecano v UD Almeria
 

Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa​

Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.Chomoka na Odds


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 
 
 

Published: 02/01/2023