2023 WM Phoenix Open 


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2023 WM Phoenix Open 

US PGA Tour

TPC Scottsdale - Stadium Course
Scottsdale, Arizona, USA 
9-12 February 2023
 
Shindano la gofu la WM Phoenix Open 2023 linatarajiwa kung’oa nanga katika mkondo wa gofu wa TPC Scottsdale uliopo Scottsdale Arizona Marekani kati ya tarehe 9 na 12 Februari.
 
Kuhusu shindano hili.  
 
Shindano hili ni sehemu ya PGA Tour na lilianza miaka 91 iliyopita ikiwa ni mwaka 1932 likijulikana kama Arizona Open lakini likasitishwa baada ya mashindano ya mwaka 1935.
 
Shindano la Phoenix Open lilirejea mwaka 1939 Bob Goldwater Sr. alipowashawishi wenzake wa kikundi cha Thunderbirds kusaidia katika kusimamia shindano hilo na kupata ufadhili kutoka kwa Waste Management, Inc. tangu mwaka 2010.
 
Rekodi iliyowekwa na Mark Calcavecchia mwaka 2001 ya kutumia matundu 72 kupata ushindi ilisawazishwa na  Phil Mickelson mwaka 2013.
 
Habari za shindano.
 
Maandalizi ya shindano la mwaka 2023 “The People’s Open” yamekamilika na linatarajiwa kuwa mojawapo ya shindano kubwa zaidi katika historia ya shindano hili.
 
Shindano litajumuisha wachezaji 18 walio katika nafasi za kwanza 20 duniani na wachezaji 38 walio katika hamsini bora duniani kwenye jedwali rasmi la gofu, (OWGR). Mabingwa 14 wa mashindano makubwa na mabingwa 5 wa FedExCup watashiriki vile vile.
 
Wanaopigiwa Upatu kushinda
 
Wachezaji wanaoshikilia nafasi za juu kwenye jedwali la dunia la gofu kwa ubora Jon Rahm (3), Tom Kim (14) na Jordan Spieth (16) ni miongoni mwa wachezaji walioonyesha nia ya kushiriki shindano la mwaka 2023.
 
Mchezaji anayeshikilia nafasi ya pili duniani Scottie Scheffler atatetea taji lake kwenye shindano hilo ambalo litajumuisha wachezaji nguli na mahiri kama vile Rory McIlroy, Justin Thomas na Patrick Cantlay.
 
Mabingwa tisa wa zamani watakaoshiriki shindano la mwaka huu ni pamoja Scheffler (2022), Webb Simpson (2020), Rickie Fowler (2019), Gary Woodland (2018), Matsuyama (2016, 2017), na J.B. Holmes (2006, 2008).
 
Zawadi
 
Zawadi za kushindania kwenye shindano hili ni dola milioni 20 za kimarekani ambapo mshindi ataondoka na dola milioni 3.6 na pia alama 500 za FedExCup.
 
Vile vile, mshindi atapewa kombe la kioo liitwalo Crystal Glass trophy.
 
Nukuu
 
“Tunafurahi kuandaa shindano linalojumuisha wachezaji bora katika mojawapo ya shindano la kusisimua katika historia ya PGA Tour,” alisema mwenyekiti wa shindano la mwaka huu Pat Williams. 
 
“Miongoni mwa washiriki ni pamoja na mabingwa watano wa mashindano sita yaliyopita, wachezaji wanaoshikilia nafasi za juu duniani, mchezaji anayeshikilia nafasi ya kwanza duniani Rory McIlroy, mabingwa kadhaa wa mashindano makubwa ya gofu na vile vile mabingwa wa FedExCup. 
 
"Vile vile, kizazi kijacho cha nyota wa mashindano ya PGA watakuwa miongoni mwa washiriki TPC Scottsdale katika mojawapo ya wiki za kusisimua.”
 

Washindi watano wa mwisho wa WM Phoenix Open


2018 - Gary Woodland - Marekani 
2019 - Rickie Fowler - Marekani 
2020 - Webb Simpson - Marekani 
2021 - Brooks Koepka - Marekani
2022 - Scottie Scheffler - Marekani
 

Shinda na Kombe la Dunia

Dunia imekusanyika kushuhudia michuano bora zaidi ya soka. Ingia kwenye Droo yetu ya Kila Siku ya Mechi ujishindie TSh 500,000 na ufurahie Free Predictor.

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway. 


 
 

Published: 02/08/2023