Hakimiliki ya picha: Getty Images
2021/22 Spanish La Liga
Matchday 25
Valencia CF v FC Barcelona
Estadio de Mestalla
Valencia, Spain
Sunday, 20 February 2022
Kick-off is at 18h15
Valencia CF na FC Barcelona watachuana vikali katika
mechi ya ligi, Uhispania Februari 20 ugani Estadio de Mestalla.
Valencia wakiwa ugenini walipoteza mechi dhidi ya Deportivo Alaves kwa 2-1. Mechi hiyo ilichezwa Februari 13.
Valencia wamepoteza mechi nne na kupata sare katika mechi mbili kati ya sita za mwisho za ligi walizocheza.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Vile vile, Valencia hawajashinda katika mechi tatu za mwisho wakiwa nyumbani. Wamepoteza mechi moja na kupata sare katika mechi mbili mfululizo ugani Estadio de Mestalla.
Kwengineko, Barcelona walitoka nyuma na kulazimisha sare ya 2-2 dhidi ya RCD Espanyol katika mechi ya ligi iliyochezwa Februari 13.
Barca, katika mechi nane zilizopita wameshinda mechi nne na kupata sare katika mechi nne.
Katika mechi nane za mwisho wakiwa wageni, Barcelona hawajapoteza mechi yoyote huku wakiambulia sare tano na ushindi mara tatu.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
"Tulitakiwa kushinda mechi hii. Tulipoimarisha mchezo wetu tulifanikiwa kufunga magoli mawili,” alisema meneja wa Barcelona Xavi Hernandez baada ya sare hiyo dhidi ya Espanyol.
"Mchezo ulipokuwa 2-1, ilionekana wazi kuwa tungepata alama moja lakini baada ya kuuchambua vizuri kwa maoni yangu tulifaa kushinda. Tulimiliki mchezo vizuri kabisa na tulitengeneza nafasi nyingi. Tulipoteza alama mbili.
"Kipindi chote cha mchezo tuliwazidi umiliki wa mpira. Walicheza mchezo wa kushtukiza na walitumia nafasi zao vizuri sana.”
Mara ya mwisho Valencia na Barcelona walipatana katika mchezo wa igi mnamo Oktoba 17 2021.
Barcelona waliitandika Valencia 3-1 katika mechi hiyo iliyochezewa ugani Camp Nou ambao ni uwanja wa nne duniani kati ya nyanja zinazobeba mashabiki wengi.
Takwimu za timu hizi katika mechi tano za ligi zilizopita
Mechi - 5
Valencia - 1
Barcelona - 2
Sare - 2
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.