Toffees kuwa wenyeji wa City Goodison Park


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021/22 English Premier League

Matchday 27

Everton v Manchester City

Goodison Park
Liverpool, England
Saturday, 26 February 2022
Kick-off is at 20h30 
 
Everton watakuwa mwenyeji wa Manchester City katika mechi ya ligi ugani Goodison Park Jumamosi Februari 26, huku City wakipania kujizoa baada ya kupoteza mechi dhidi ya Tottenham Hotspurs.
 
The Citizens walipoteza mechi dhidi ya Tottenham Spurs 3-2 wakiwa nyumbani katika hali ya kushangaza mnamo Februari 19 huku matokeo hayo yakivunja msururu wa mechi 15 bila kupoteza mechi yoyote. Walipata ushindi katika mechi 14 kati ya hizo 15.
 
Wapinzani wa karibu ambao ni Liverpool walipunguza alama kati yao hadi alama sita huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi. Mkufunzi Pep Guardiola atawataka wachezaji wake kumaimarisha mchezo wao na kupata matokeo mazuri watakapokutana na Everton.

Pep Guardiola
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Guardiola kwa kipindi kimoja alisisitiza ugumu uliopo katika katika kutetea taji la ligi nchini England lakini anasema timu yake itazidi kupambana katika mechi 12 zilizosalia wakiwa na matumaini ya kulitetea taji hilo.
 
"Ni jambo la kawaida kupoteza mechi hasa katika ligi ya premier. Timu zote zilizopo katika nafasi za chini kwenye jedwali zilishinda wikendi hii,” Guardiola alisema baada ya mchezo na Tottenham.
 
"Kila timu inapambania kila taji na huo ndio ugumu wa uzuri wa ligi hii. Chochote kinaweza kutokea na tumeshuhudia hilo leo. Tumepoteza mechi ambayo tulikuwa karibu sana kupata sare na hata pengine ushindi. Pongezi kwa Tottenham.
 
"Tutapumzika wiki hii kabla ya mchezo unaofuata. Tutapambana katika mechi zote kwa nia ya kupata ushindi. Tunahitaji alama nyingi ili kupata ubingwa na tutajaribu kufanya hivyo.”
 
The Toffees walipoteza mechi yao ya 13 ya ligi msimu huu baada ya kupoteza mechi dhidi ya Southampton 2-0 ugani St. Mary’s siku hiyo.
 
Ulikuwa ni mchezo wa pili wa Frank Lampard kupoteza tangu alipoirithi mikoba ya Rafael Benitez mwezi uliopita, na sasa Everton wapo kwenye nafasi ya 16, alama nne juu ya nafasi ya kushushwa daraja.

Frank Lampard
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Lampard amekiri kwamba timu hiyo inahitaji kuimarisha matokeo ya mechi za ugenini na kuongeza kuwa kuna mambo Fulani ya kufanyia kazi katika mazoezi.
 
"Tumeimarika zaidi tangu nimechukua usukani lakini bado kuna nafasi ya kuimarika zaidi hasa katika mechi za ugenini. Nyumbani tumeonyesha uwezo mkubwa tofauti na ugenini,” alisema.
 
"Wachezaji wangu hawakuonyesha ujasiri wa kujinasua baada ya wapinzani kutukaba. Huo ndio wasiwasi wangu mkubwa na ni jambo la kufanyia kazi.
 
"Itachukua muda kuyafanyia kazi mapungufu haya. Tunahitaji kukuza uwezo wa kucheza katika mazingira yoyote hata kwenye shiniko kubwa wakati wowote. Kuna makosa niliyoyaona leo na tutayafanyia kazi.”
 

Takwimu baina ya timu hizi katika mechi 5 za mwisho za ligi.

 
Mechi - 5
Everton - 0
Man City - 5
Sare - 0


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.


 

Published: 02/23/2022