Senegal wapania taji la AFCON kwa mara ya kwanza dhid ya Misri


Hakimiliki ya picha: BackpagePix

 

2021 Africa Cup of Nations (AFCON)

Final

Senegal v Egypt 

Stade Omnisport Paul Biya 
Yaounde, Cameroon 
Sunday, 6 February 2022
Kick-off is at 22h00  
 
Senegal na Misri watapambana katika mechi kali ya fainali kusaka mshindi wa taji la AFCON 2021 katika uwanja wa Omnisport Paul Biya Februari 6. 
 
The Lions of Teranga, kama inavyofahamika timu ya taifa ya Senegal walifika fainali hii baada ya kuichapa Burkina Faso 3-1 katika mechi ya nusu fainali iliyoandaliwa Februari 2.  
 
Hadi kufikia wakati huu wa shindano hili la AFCON, Senegal hawajapoteza mchezo wowote huku wakipata ushindi katika mechi nne na sare katika mechi mbili. 

Mohamed Salah
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Senegal hawakuanza shindano hili vyema baada ya kupata sare mbili dhidi ya Guinea na Malawi kabla ya kupata ushindi dhidi ya Zimbabwe katika mechi za kundi B. 
 
Baada ya mwanzo mgumu, vijana hao wanaofundishwa na Aliou Cisse wameshinda mechi tatu mfulululizo, ikiwa ni dhidi Cape Verde, Equitorial Guinea na Burkina Faso.
 
"Hiki ni kiashiria kwamba tumaimarika zaidi. Tulifahamu fika kwamba haingekuwa rahisi kufika hatua ya fainali ya AFCON mara mbili mfululizo,” mchezaji nyota wa Senegal Sadio Mane alisema baada ya ushindi dhidi ya Burkina Faso.
 
"Jambo la msingi kwetu sasa ni kushinda taji lenyewe kwa kumshinda yeyote tutakaye kutana naye. Burkina Faso wamekuwa wapinzani wakali na wametupa ushindani mkubwa. 
 
"Inaonyesha usoni mwangu furaha niliyo nayo. Kwa kweli nastahili kuwa na furaha. Nina furaha kubwa sana binafsi, kwa wachezaji wenzangu na taifa langu.” 
 
Hii ni mara ya tatu taifa la Senegal kufika hatua ya fainali ya AFCON na imani ni kubwa kwanza safari hii wataibuka na ushindi. 
 
Mwaka 2002, Senegal walishindwa na Cameroon 3-2 kwa njia ya matuta ya penalti nchini Nigeria kabla ya kupoteza fainali dhidi ya Algeria,1-0 mwaka 2019 kule nchini Misri. 
 
Hii itakuwa mara ya 13 katika mechi zote timu hizi kukutana.
 
Misri imeonyesha ubabe wake dhidi ya Senegal kwa kushinda mechi sita kati ya kumi na tatu walizocheza, Senegal wakishinda nne huku mechi mbili zikiishia sare. 
 
Mechi ya mwisho baina ya Senegal na Misri ilikuwa mnamo Novemba 15 2014. 
 
Ilikuwa ni mechi ya kufuzu shindano la AFCON 2015 iliyochezewa ugani Cairo International Stadium, Cairo, ambapo Senegal iliibuka na ushindi wa 1-0. 
 

Takwimu baina ya Senegal na Misri katika mechi zote walizokutana

Mechi - 12
Senegal - 2
Misri - 6
Sare - 4


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 02/04/2022