Rodgers kuja na mbinu za kuwaangamiza waajiri wa zamani


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021/22 English Premier League

Matchday 24

Liverpool v Leicester City

Anfield
Liverpool, England
Thursday, 10 February 2022
Kick-off is at 22h45  
 
Leicester wanatazamia kuwashinda Liverpool kwa mara ya pili msimu huu katika mechi za ligi watakapokutana Februari 10 uwanjani Anfield.
 
Katika mechi ya mkondo wa kwanza, Leicester waliishinda Liverpool 1-0 ugani King Power Stadium mnamo Disemba 28 2021 ikiwa ni ushindi wa pili wa Rogers dhidi ya Liverpool akiwa na Leicester.
 
Leicester wamecheza mechi mbili za ligi tangu mechi hiyo kutokana na wimbi la virusi vya Covid-19 lililoathiri ratiba ya mechi katika kipindi cha krismasi.
 
Vijana hao wa Brendan Rogers walipoteza 3-2 dhidi Tottenham na kufuatisha sare ya 1-1 dhidi ya Brighton mechi zote wakiwa nyumbani, matokeo ambayo yalipelekea timu hiyo kuwa katika nafasi ya kumi na alama 26.

Brendan Rodgers
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Rodgers aliwasifia wachezaji wake kwa kuwadhibiti wapinzani japokuwa waliruhusu goli nyakati za mwisho za mchezo, na kuwaasa kuwa wavumilivu wanapomiliki mpira.
 
"Tuliruhusu goli nyakati za mwisho leo. Bila kujiamini ingekuwa rahisi kukata tamaa lakini tulijikaza. Wachezaji wangu walijituma sana,” alisema Rodgers baada ya mechi hiyo.
 
"Bado naamini kwamba kuna maeneo ya tunayoweza kuimarika. Hatumiliki mpira kwa muda tunaostahili. Ni jambo ambalo tumekuwa tukifanyia mazoezi kwa muda mrefu.
 
"Wakati mwingine wachezaji wanakuwa na haraka ya kushambulia badala ya kuwa watulivu na kutafuta nafasi mwafaka. Tukifanya hivyo tunaonyesha weledi wetu lakini leo tulipoteza mpira mara nyingi na kujiletea shinikizo.”
 
Liverpool kwa upande wake wamerudisha matumaini ya kushinda taji la premier baada ya kuishinda Brentford 3-0 kisha kuishinda Crystal Palace 3-1. Hii ni baada ya kupoteza alama muhimu dhidi ya Tottenham, Leicester na Chelsea hivi maajuzi.
 
Kwa ushindi dhidi ya Crystal Palace, Liverpool walipunguza nafasi baina yake na viongozi Manchester City kuwa alama tisa huku City wakiwa na mchezo mmoja zaidi.

Jurgen Klopp
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Klopp alisema kuwa mchezo haukuwa mzuri sana Selhurst Park baada ya dakika 35 kutokana na mrundikano wa ratiba.
 
"Ulikuwa ni mchezo wa kupanda na kushuka. Tulidhihirisha uwezo wetu na tulionyesha mchezo mzuri dakika za kwanza 35,” alisema mjerumani huyo baada ya mechi hiyo.
 
"Baada ya wiki yenye shughuli nyingi, tulikuwa na mechi kubwa dhidi Arsenal ugenini na kusafiri nyumbani tena, kisha tukaja hapa. Nahisi uchovu ndio sababu ya mchezo tulioonyesha leo.
 
"Tulilegea kidogo katika safu yetu ya ulinzi. Tuliwapa nafasi nyingi za kutushambulia katika kipindi cha kwanza kutokana na maamuzi duni. Kipindi cha pili kulikuwa na utepetevu kwa upande wetu vile vile kwa sababu hatukuzuia vizuri.
 
"Walibuni mbinu ya kutushambulia kwa kucheza pasi ndefu. Mchezo ulifunguka zaidi na ilitubidi kuongeza nguvu zaidi jambo ambalo tulifanya. Kwa kifupi tulicheza vizuri dakika 35 tu. Sehemu nyingine ya mchezo hatukuwa vizuri.”
 

Takwimu baina ya Liverpool na Leicester katika mechi tano za mwisho za ligi

 
Mechi - 5
Liverpool - 3
Leicester - 2
Sare - 0


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 02/01/2022