Red Devils kuendeleza ubabe wao dhidi ya the Saints


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021/22 English Premier League

Matchday 25

Manchester United v Southampton

Old Trafford
Manchester, England
Saturday, 12 February 2022
Kick-off is at 15h30  
 
Manchester United watanuia kuendeleza ubabe wao dhidi ya Southampton watakapokutana katika mechi ya ligi ugani Old Trafford Jumamosi Februari 12.
 
The Red Devils hawajapoteza mechi yoyote dhidi ya Southampton tangu January 2016 walipopoteza 1-0 ugani Old Trafford, na sasa ni mechi kumi na moja za ligi kutoka wakati huo.
 
Msimu uliopita, Manchester United walishinda mechi zote mbili za ligi, ugenini na nyumbani ambapo walifunga mabao 9 miezi kumi na mbili iliyopita.
 
Miamba hao wa soka wa England walitolewa katika shindano la FA kwenye hawamu ya nne na Middlesbrough kwa njia ya matuta baada ya dakika 120 na sare ya 1-1 ugani Old Trafford.

Ronaldo
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Meneja wa mpito wa United Ralf Rangnick alikiri kwamba walijutia sana nafasi walizokosa, ikiwa ni pamoja na Bruno Fernandes kugonga chuma katika kipindi cha pili lango likiwa wazi.
 
“Nahisi tumekuwa tukicheza vizuri wiki zilizopita, katika ligi na leo vile vile katika kipindi cha kwanza,” alisema Rangnick baada ya mechi na Middlesbrough.
 
"Sidhina tungefanya zaidi ya tulivyofanya leo zaidi ya kufunga magoli zaidi kipindi cha kwanza. Ni sharti tutumie nafasi zetu kwa umakini tunapozipata. Leo hatukufanya hivyo.
 
“Nafasi aliyopata Bruno, anaweza kufunga nafasi tisa kwa kumi anapopata nafasi kama hizo katika mchezo. Leo amekosa nafasi hiyo. Nadhani alijaribu kuuweka mpira wavuni kwa njia ya kipekee.
 
"Chochote kinaweza kutokea. Hakufanya hivyo kwa kupenda na sasa tunachotakiwa kufanya ni kuangazia macho katika mashindano mwawili yaliyosalia.”

Ralph Hasenhuettl
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Kocha wa Southampton Hasenhuttl na vijana wake walipata ushindi wa 2-1 dhidi ya Coventry kwenye muda wa ziada katika mechi ya FA mnamo Februari 5. Mechi iliandaliwa St. Mary’s na mjerumani huyo alisema vijana wake walikosa kasi kutokana na mapumziko ya hivi majuzi.
 
"Tumetoka katika mapumziko ya wiki mbili kwa hivyo ni kawaida tulikosa kasi katika kipindi cha kwanza,” alisema baada ya mechi hiyo ya FA.
 
"Tulipofanya mabadiliko ya wachezaji mchezo wetu uliimarika na tukaanza kutengeneza nafasi. Haikuwa rahisi dhidi yao lakini mwishowe tulifanikiwa kufunga mabao mawili.
 
"Tulipambana vizuri bila kusahau mpira aliouokoa Willy Caballero. Tulipigana vilivyo kupata kupata ushindi wa leo.”
 

Matokeo baina ya timu hizi katika mechi tano za mwisho za ligi

Mechi - 5
Man United - 2
Southampton - 0
Sare - 3

Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 02/09/2022