Napoli kutoana kijasho na Inter


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021/22 Italian Serie A 

Matchday 25

SSC Napoli vs Inter Milan 

Estadio Diego Armando Maradona 
Naples, Italy 
Sunday, 12 February 2022
Kick-off is at 20h00  
 
SSC Napoli watakuwa mwenyeji wa Inter Milan ugani Stadio Diego Armando Maradona katika mechi ya ligi Februari 12.
 
The Little Donkeys, ambao ni Napoli walipata ushindi wa 2-0 wakiwa nyumbani dhidi ya Venezia katika mechi iliyochezwa Februari 6.  
 
Napoli hawajapoteza mechi katika mechi tano zilizopita za ligi huku wakishinda mechi nne mfululizo na kupata sare moja.

Fabian Ruiz
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Vile vile, Napoli hawajapoteza mechi yoyote katika mechi mbili wakiwa nyumbani huku wakipata ushindi wa mechi zote mbili kama mwenyeji.
 
Kwingineko, Inter walipoteza mechi yao dhidi ya AC Milan kwa 2-1 wakiwa nyumbani mnamo Februari 5.
 
Inter Milan walipoteza msururu wa mechi 14 za ligi bila kushindwa baada ya kushindwa na AC Milan. Walikuwa wameshinda mechi 11 na kupata sare katika mechi 3.
 
Hata hivyo, Inter Milan hajapoteza mechi hata moja kati ya sita zilizopita za ugenini huku wakiandikisha ushindi mara nne na kupata sare 2.

Ismael Bennacer
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
"Kwa maoni yangu tulicheza kama kawaida yetu; nguvu, ujasiri na udhabiti,” alisema nahodha wa Inter Samir Handanovic baada ya kupoteza dhidi ya AC Milan.
 
"Ukiachia mbali nyakati za mwisho za mechi hiyo, tutakaa na tuchambue wapi tulikosea na tutafute mbinu za kurekebisha. Nyakati tofauti za mechi tulifanya maamuzi ya ovyo yaliyopelekea kupoteza mpira.
 
"Hayo yamepita na sasa macho yetu yapo katika mechi ya Coppa Italia dhidi ya Roma kisha tutacheza dhidi ya Napoli na Liverpool. Mechi ni nyingi na zinakuja kwa kasi. Tutachambua makossa yetu na tuendelee na safari. Akili zetu zipo katika mechi ijayo.”
Napoli na Inter Milani walikutana mwisho katika mechi ya ligi mnamo Novemba 21 2021.
 
Inter wakiwa nyumbani, Stadio Giuseppe Meazza, maarufu kama San Siro waliishinda Napoli 3-2.  
 

Takwimu baina ya timu hizi katika mechi 5 za mwisho za ligi

Mechi - 5
Napoli - 0
Inter - 4
Sare - 1


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.


Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 
 

Published: 02/09/2022