Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022 AT&T Pebble Beach Pro-Am
US PGA Tour
Pebble Beach, California, USA
3-6 February 2022
Shindano la
2022 AT&T Pebble Beach Pro-Am la golfu litachezwa kwenye mikondo mitatu tofauti kati ya tarehe 3 na 6 Februari.
Mikondo hiyo mitatu inajumuisha Pebble Beach Golf Links, Spyglass Hill Golf Course na Monterey Peninsula Country Club.
Shindano hilo liliasisiwa mwaka 1937 na AT&T Corporation ikawa mdhamini wa taji lake mwaka 1986 ambayo ni miaka 36 iliyopita.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Daniel Berger ndiye bingwa mtetezi wa shindano hilo la AT & T Pebble Beach Pro-Am baada ya kuibuka mshindi mwaka uliopita.
Berger atakuwa miongoni mwa washiriki 156 wa shindano hilo litakalochukua siku nne huku likiwa ni shindano la 14 katika ratiba ya 2021/22 ya PGA Tour.
Baadhi ya washiriki wa shindano la mwaka huu ni pamoja na Jordan Spieth, Matt Fitzpatrick, Davis Love III, Kevin Kisner, Justin Rose na wengineo.
Washindi wa zamani wa AT&T Pebble Beach Pro-Am Peter Jacobsen, Ted Potter Jr, na Nick Taylor vile vile watashiriki wakinuia kushinda shindano hilo kwa mara nyingine.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
“Mauzo ya tiketi yamekuwa juu na watu wengi wananuia kuhudhuria. Kwa ujumla, mchezo wa golfu umerudi katika ubora wake,” alisema mkurugenzi mtendaji wa AT&T Pebble Beach Pro-Am na mkrugenzi wa shindano hilo Steve John.
"Litakuwa ni shindano zuri na la kuvutia kwa kila atakayehudhuria. Watu wapya mashuhuri watakuwepo; Mia Hamm, Cornell Alvarez, Lucas Nelson.
“Mauzo ya tiketi ya mwaka huu peke yake yamezidi mashindano mengine yaliyopita, kiashiria kwamba mashabiki wana uchu kuona mchezo wa golfu ukirudi.”
Phil Mickelson na Mark O'Meara ni wachezaji wenye mafanikio makubwa katika historia ya mashindano ya AT&T Pebble Beach Pro-Am huku wakiwa wameshinda mara tano kila mmoja.
Washindi 5 wa mwisho wa AT&T Pebble Beach Pro-Am.
2017 - Jordan Spieth - Marekani
2018 - Ted Potter Jr - Marekani
2019 - Phil Mickelson - Marekani
2020 - Nick Taylor - Canada
2021 - Daniel Berger - Marekani
Bashiri Gofu na Betway
Ingia uwanjani mchomo mmoja ubashiri gofu na Betway. Betway inakuletea matukio yote ya gofu kutoka michuano mikubwa Duniani kote.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za Facebook, Twitter, Instagram na Youtube. Pakua App ya Betway.