Knicks na 76ers kufufua uhasama wao


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

New York Knicks v Philadelphia 76ers

2021-22 NBA Regular Season

Sunday 27 February 2022

Madison Square Garden, New York City, New York

Tip-off at 21:00  
 

The New York Knicks na Philadelphia 76ers watafufua uhasama wao kwenye mechi ya NBA katika ukumbi wa Madison Square Garden, New York City jioni ya Februari 27 2022 Jumapili. Mechi inatazamiwa kung’oa nanga majira ya saa mbili kamili saa za Afrika ya kati.

The Knicks wanapambana kabisa kumaliza kumi bora ya Eastern Conference na kujiweka katika nafasi ya kucheza mechi za muondoano lakini matokeo yao ya hivi majuzi yanaashiria hali tofauti, jambo linalompa kiwewe Julius Randle kwani wamekuwa wakipoteza mechi kiholela.  

Joel Embiid
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 

“Tunapoteza mechi ambazo tunafaa kuwa tukishinda,” alisema Randle baada ya kupoteza mechi ya wiki iloyopita dhidi ya Oklahoma City Thunder. “Mechi tano zilizopita tulipaswa kushinda.”

Kwa upande wake, Philadelphia wanapigania kumaliza katika nafasi za juu za Eastern Conference na kuwaondoa kileleni Miami Heat, Chicago Bulls, Cleveland Cavaliers na Milwaukee Bucks.

The 76ers wanajivunia mojawapo ya wachezaji bora kabisa wa NBA ambaye ni James Harden aliyetokea Brooklyn Nets na mchezaji huyo mwenye miaka 32 anasema kuwa anatazamia kushinda taji na timu yake mpya.

Kemba Walker
Hakimiliki ya picha: Getty Images


“Lengo ni kushinda taji. Hilo ndilo lengo letu,” alisema Harden. “Kama alivyosema Daryl Morey, muda wa kushinda ni sasa. Joel Embiid amekuwa akicheza vizuri sana. Kazi yangu ni kumsaidia na kuisaidia timu kushinda taji mwaka hu una miaka ya usoni.” [

“Mimi na Embiid tunaelewana sana uwanjani. Uwezo wa Embiid unaeleweka sana na unafahamika. Sio kwa kufunga tu bali pia kuwasaidia wenzake kufunga. Uwepo wake ni pigo la kisaikolojia kwa wapinzani,” aliongeza.

Takwimu baina ya timu hizi inaonyesha wamekutana mara 462 tangu mwaka 1949-50; Philadelphia wakishinda mara 259 ikilinganishwa na 203 kwa faida ya Knicks. Mara ya mwisho kukutana kwa timu hizi ilikuwa Novemba 2021, Knicks walishinda 103-96 wakiwa ugenini huku Julius Randle akichangia alama 31.
 

Takwimu baina ya New York Knicks na Philadelphia 76ers

Michezo: 462

Knicks: 203

76ers: 259
 

Bashiri Mpira wa Kikapu na Betway


Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni mpira wa miguu, mpira wa kikapu, rugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.




Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.

Published: 02/25/2022