Hakimiliki ya picha: Getty Images
2021/22 Italian Serie A
Matchday 26
Juventus FC v Torino FC
Allianz Stadium
Torino, Italy
Friday, 18 February 2022
Kick-off is at 22h45
Juventus FC watakuwa mwenyeji wa Torino ugani Allianz Stadium katika
mechi ya ligi mnamo Februari 18.
Juventus walichezea sare ya 1-1 na Atlanta BC wakiwa ugenini katika mchezo wa ligi uliopita wa tarehe 13 Februari.
Kwa sasa, Juventus wamecheza mechi kumi na moja za ligi bila kushindwa huku wakiambulia ushindi mara saba na kupata sare nne.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Vile vile, Juventus hawajashindwa katika mechi tano za ligi za mwisho wakiwa nyumbani huku wakipata sare moja na ushindi katika mechi nne.
Kwengineko, Torino walichezea kichapo cha 2-1 dhidi ya Venezia wakiwa nyumbani katika mechi iliyopita ya tarehe 12 Februari.
Kutokana na matokeo hayo, Torino hawajashinda mechi yoyote katika mechi tatu za ligi zilizopita; wakiambulia sare moja na kuchapwa katika mechi mbili mfululizo.
Wakiwa ugenini, Torino wamepoteza mechi mbili na kushinda moja dhidi ya Sampdoria.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
“Dakika za kwanza 20 tulikuwa na mchezo mzuri. Venezia walibadilisha mfumo na kutumia 3-4-3. Walitudhibiti na nafasi tulizokuwa tunatengeza zilibanwa,” alisema meneja wa Torino Ivan Juric baada ya kushindwa na Venezia.
"Mchezo wao uliimarika kabisa na walitufunga mara baada ya kipindi cha pili kuanza. Wachezaji wetu walijituma sana lakini wakakosa umakini wa kumaliza nafasi hizo. Venezia walizuia sana baada ya kupata mabao.
"Walikuwa na mchezo mzuri kwa dakika 20 na tulisumbuka sana kudhibiti mipira mifu, hatukuweza kutengeneza nafasi muda huo, shinikizo lilizidi kwa upande wet una ilikuwa vita. Tunawapa pongezi Venezia kwa kupata ushindi.”
Timu hizi zilikutana mara ya mwisho katika mechi ya ligi iliyochezwa mnamo Oktoba 2 2021.
Juventus walipata ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Torino ugani Olimpico Grande, Torino.
Takwimu baina ya timu hizi katika mechi tano za ligi za mwisho
Mechi - 5
Juventus - 4
Torino - 0
Sare - 1
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.