Hakimiliki ya picha: Getty Images
2021/22 UEFA Champions League
Round of 16 - First-Leg
Inter Milan v Liverpool FC
Stadio Giuseppe Meazza
Milano, Italy
Wednesday, 16 February 2022
Kick-Off 23h00
Inter Milan na Liverpool watamenyana katika mchezo wa
ligi ya mabingwa raundi ya 16 mnamo Februari 16.
Mabingwa hawa wa Italia walifuzu kuingia raundi hii baada ya kumaliza katika nafasi ya pili ya kundi D nyuma ya miamba wa Uhispania Real Madrid.
Inter Milan walipoteza mchezo wao wa mwisho wa kundi D 2-0 wakiwa ugenini dhidi ya Madrid. Matokeo hayo yalifikisha kikomo msururu wa mechi nne kwa Inter bila kushindwa katika mashindano haya.

Hakimiliki ya picha: Getty Images
Hata hivyo, Inter hawajapoteza mechi yoyote kati ya mechi mbili za mashindano haya wakiwa nyumbani huku wakiandikisha ushindi mfululizo katika mechi mbili.
Liverpool kwa upande mwingine waliingia katika raundi ya 16 baada ya kushinda kundi B wakifuatiwa na Atletico Madrid katika nafasi ya pili.
The Reds walishinda mchezo wao wa mwisho wa kundi B wakiwa ugenini kwa mabao 2-1 dhidi ya wapinzani wa jadi wa Inter Milan, AC Milan mnamo Disemba 7 na kuendeleza ushindi kuwa wa mechi saba bila kushindwa katika shindano hili.
Vile vile, Liverpool hawajapoteza mchezo wowote katika mechi tatu za mwisho wakiwa ugenini katika shindano hili huku wakishinda mechi zote tatu kwa mpigo.

Hakimiliki ya picha: Getty Images
"Ndio, tunawaelewa Alexis Sanchez na Edin Dzeko vizuri sana bila kumsahau Lautaro Martinez ambaye pengine ni mmoja kati ya washambulizi hatari duniani,” alisema Jurgen Klopp wa Liverpool baada ya kupewa wapinzani hao kwenye kumi na sita bora.
"Simone Inzaghi ndiye mkufunzi ukiwa ni mwaka wa kwanza. Mwaka jana walikuwa mabingwa lakini hii Liverpool haichagui wapinzani kwa hivyo haitakuwa rahisi kwao. Inawezekana na tutajaribu. Utakuwa ni mchezo wa kusisimua na tunautazamia sana.
"Ni mechi ngumu kwa kweli. Ni viongozi wa ligi nchini Italia na ni timu nzuri. Tusubiri kuona mambo yatakuwaje ifikiapo Februari.”
Mara ya mwisho Inter na Liverpool kukutana katika mechi ya ligi ya mabingwa ilikuwa Novemba 3 2008.
Liverpool walishinda mechi hiyo 1-0. Mchezo huo ulichezewa ugani Stadio Giuseppe Meazza katika mji wa Milan.
Takwimu baina ya timu hizi katika mechi ya UEFA
Mechi - 4
Inter - 1
Liverpool - 3
Sare - 0
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.