Inter Milan na AC Milan kumenyana katika debi


Hakimiliki ya picha: Getty Images
 

Italian Serie A

Matchday 24

Inter Milan v AC Milan

San Siro
Milan, Italy
Saturday, 5 February 2022
Kick-off is at 20h00 
 
AC Milan wanapania ushindi dhidi ya Inter milan watakapokutana katika debi ya della Madonnina ugani San Siro Jumamosi Februari 5, ambao utakuwa ni mchezo wa 230 baina ya timu hizi mbili. 
 
The Rossoneri, hawajawa na mafanikio makubwa dhidi ya wapinzani wao wa jadi huku wakishinda mara moja tu katika mechi tano za ligi zilizopita nao Nerazzuri wakishinda mara tatu.  
 
Vijana wa Stefano Pioli wanaingia katika mechi hii baada ya kutoka sare ya 0-0 dhidi ya Juventus, mechi iliyochezwa Januari 23. Kabla ya hapo, walikuwa wamepoteza mechi dhidi ya Spezia siku sita zilizopita.
 
Kwa sasa Milan wapo katika nafasi ya tatu na alama 49 wakiwa na mchezo mmoja zaidi ya Inter ambao wamewaacha na alama nne. 

Stefano Pioli
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Pioli amekiri kwamba alama moja walioipata dhidi ya Bianconeri ni muhimu sana katika mbio za ubingwa ukizingatia Napoli wapo katika nafasi ya pili wakifukuzia ubingwa. 
 
"Tupo hapa tulipo kutokana na alama tulizopoteza dhdi ya Spezia na sio kutokana na mchezo wa leo. Vijana wetu wanafahamu fika mechi dhidi ya Juventus na Inter zitakuwa na athari katika nafasi yetu mwisho wa ligi,” aliambia DAZN baada ya mechi na Juventus. 
 
"Iwapo tutashinda mechi dhidi ya Inter bado tutakuwa karibu nao. Tukifeli basi itakuwa kama msimu jana ambao tulimaliza katika nafasi ya pili katika siku ya mwisho ya ligi, ambayo tungemaliza hata katika nafasi ya tano.” 
 
Januari 22, Inter waliishinda Venezia 2-1 na kuendeleza msururu wa mechi 14 bila kushindwa tangu walishindwa 3-1 tarehe 16 Oktoba na Lazio, ambapo ndiyo mechi ya pekee waliyopoteza msimu huu. 

Simone Inzaghi
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Kocha mkuu Simone Inzaghi alisisitiza kuwa ni muhimu kuendeleza msururu huo huku wakipigania ubingwa katika mashindano matatu. 
 
"Ushindi wa leo ni zaidi ya alama tatu kwa sababu tumeshinda mechi tisa na kutoa sare moja katika mechi kumi zilizopita,” alisema Inzaghi walipoishinda Venezia. 
 
"Tumefuzu kuingia roundi inayofuata ya ligi ya mabingwa na Coppa Italia na tayari tumeshinda Super Cup. Ni viashiria vizuri. Lengo letu ni kuzidi kupambana katika mashindano yote japokuwa itazidi kuwa vigumu kila uchao. 
 
"Tutasherehekea kwa sasa, tupumzike kidogo kisha Jumatano tutaanza mazoezi na wachezaji wetu ambao hawajaitwa kuwakilisha mataifa yao ili kujiweka tayari kwa debi.” 
 

Takwimu baina ya Inter Milan na AC Milan katika mechi 5 za mwisho za ligi

 
Mechi - 5
Inter Milan - 3
AC Milan - 1
Sare - 1


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.

Published: 02/03/2022