Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022 The Honda Classic
US PGA Tour
PGA National Resort & Spa - The Champion Course
Palm Beach Gardens, Florida, USA
24-27 February 2022
Rickie Fowler anatazamia kuiga mfano wa wachezaji wanne wakubwa wa golfu kwa kushinda
Honda Classic katika jimbo la Florida, Marekani mnamo Februari 27.
Mmarekani huyo atakuwa mchezaji wa tano kushinda shindano hili kwa mara ya iwapo atafanikiwa kulishinda wikendi hii baada ya kuchukua nafasi ya pili mwaka 2019 na nafasi ya sita 2016.
Jack Nicklaus, Johnny Miller, Mark Calcavecchia na Pádraig Harrington ndio wachezaji wanne walioshinda taji hilo zaidi ya mara moja.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Mchezaji huyo aliyezaliwa California alishinda Honda Classic katika shindano lake la nne la PGA Tour mwaka 2017 kwa kumshinda Gary Woodland na Morgan Hoffmann.
Kwa mara ya kwanza katika mchezo huu, Fowler alilinda ushindi wake baada ya kuongoza kwa matundu 54 na kushinda taji hilo, ushindi ambao ulipelekea kukwea katika kumi bora kwenye jedwali la golfu duniani.
Fowler alishinda shindano la Waste Management Phoenix Open mwaka 2019 baada ya kuongoza na kupoteza alama chache kisha kuchukua uongozi tena na baadaye kushinda shindano hilo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 alimaliza katika nafasi ya nane katika PGA Tour yam waka 2021 na hii ilikuwa ni mara yake ya 12 kumaliza kumi bora katika shindano kubwa huku akitazamia kushinda taji la kwanza baada ya kushinda Phoenix Open.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Fowler ambaye ameshinda mashindano tisa katika Maisha yake ya mchezo, hivi majuzi alisema anajihisi vizuri na anatarajia kushinda mataji zaidi mwaka 2022.
“Zaidi imekuwa kuingia uwanjani na kufurahia mchezo ninapocheza,” alisema Fowler.
“Ni faraja kubwa kuweza kuingia uwanjani na kucheza mchezo wa golfu. Kama nilivyosema awali, cha msingi ni kufanya mazoezi kikamilifu bila kujali mambo mengi.
"Imekuwa safari ndefu lakini nilikuwa na imani matokeo mazuri yatakuja. Inafariji kuona matunda yake.”
Washindi watano wa mwisho wa The Honda Classic.
2017 - Rickie Fowler - Marekani
2018 - Justin Thomas - Marekani
2019 - Keith Mitchell - Marekani
2020 - Im Sung-Jae - Korea Kusini
2021 - Matt Jones - Australia
Bashiri Gofu na Betway
Ingia uwanjani mchomo mmoja ubashiri gofu na Betway. Betway inakuletea matukio yote ya gofu kutoka michuano mikubwa Duniani kote.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za Facebook, Twitter, Instagram na Youtube. Pakua App ya Betway